HOME

May 22, 2013

GHARAMA ZA ZIARA ZA RUTTO KUCHUNGUZWA!!


Gazeti la nation Kenya limeripoti kuwa, Ziara ya Naibu Rais wa Kenya William Ruto katika nchi za Magharibi na Afrika ya Kati imeibua mtafaruku mkubwa katika bunge la nchi hiyo na sasa uchunguzi wa gharama za ziara hiyo utafanyika.

Baadhi ya wabunge wametaka kuchunguzwa kwa kina ziara hiyo iwapo ilikuwa ni ya lazima, ikiwa ni pamoja na gharama zilizotumika kwa kutumia fedha za walipakodi.

Uchunguzi huo utatakakubaini kwanini kulikuwa na ulazima wa
kukodi ndege ya ziara hiyo kwa ajili ya Ruto, na ni kiasi gani kilitumika kwa yeye na ujumbe waliosafiri nae.

No comments:

Post a Comment