Baadhi ya wabunge wa Tanzania wameitka serikali kuhakikisha inaweka mikakati ya kuwatosha kuwakomboa vijana katika suala la ajira na kuwawezesha kupata mikopo ili kuweza kujiunga na ujasiriamali utakaowawezesha kujikomboa na umaskiuni.
Wakichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya habari, vijana utamaduni na michezo bungeni mjini Dodoma, Wabunge hao akiwemo Mhe. Nassib Omary na Stepheni Wassira wamesema ni vyema serikali ikaongeza bajeti na kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya kuwawezesha vijana kupata mikopo rahisi yenye riba nafuu.
Awali wakati akisoma makadirio ya bajeti ya Wizaya ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Waziri wa wizara hiyo Mhe. Fenela Mukangara amesema serikali imekuwa ikishirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo katika kutekeleza shughuli mbali mbali za maendeleo ya vijana hapa nchini.
Amsema imeweka mikakati mbalimbali ya kuwakomboa vijana ikiwemo utaratibu wa uanzishwaji wa benki ya vijana ambayo mchakato wake unaendelea kuwajengea vijana utaalamu wa kijasiriamali.
Akiwasilisha maoni ya Kamati ya Bunge kuhusu Wizara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mohamed Mtanda amesema ipo haja ya serikali kusaidia vijana kupata ajira kwa kuwawezesha kupata mikopo kutoka mabenki mbalimbali.
No comments:
Post a Comment