HOME

May 23, 2013

MZEE WA MIAKA 80 AVUNJA REKODI KUFIKA KILELE CHA MLIMA EVEREST!!

Mzee mwenye umri wa miaka 80 raia wa Japan amefanikiwa kufika kilele cha mlima  Everest kwa mujibu wa timu yake na kumfanya kuwa mwanaume mzee kuliko wote kufika kilele cha mlima huo mrefu kuliko yote duniani.

Kwa mujibu wa timu yake, Yuichiro Miura ambaye alipanda mlima Everest akiwa na umri wa miaka 70 na mara nyingine akiwa na umri wa miaka 75 alifika kilele cha mlima huo mapema siku ya Alhamis asubuhi.

Yuichiro anachukua nafasi ya Bahadur Sherchan ambaye
alifika kilele cha mlima huo akiwa na umri wa miaka 76 mwaka 2008 na kushikilia rekodi hiyo.

No comments:

Post a Comment