HOME

May 22, 2013

BREAKING NEWS! AJALI MBAYA YA GARI BARABARA YA CHANG'OMBE DAR ES SALAAM!!



Ajali mbaya inayohusisha magari matatu imetokea katika barabara ya Chang'ombe jijini Dar es salaam na kusababisha msongamano mkubwa wa magari na watu kuchota mafuta yanayomwagika kutoka kwenye Lori hilo.

Kwa mujibu wa ripoti kupitia East Afrika Radio kipindi cha Supamix na shuhuda wa ajali, Lori T219 likiwa limetoka bandarini kwenda Ubungo limegonga daladala na kupinduka na kuziba barabara ya Chang'ombe.

Hakuna mtu ambaye amepoteza maisha mpaka sasa lakini taarifa zaidi za majeruhi zitakujia hapo baadae ambapo sehemu kubwa ya barabara imejaa mafuta ya mawese watu wanajichotea.

Hatari iliyopo ni kwamba ni kwamba kutokana na watu kuchota mafuta yanayomwagika kutoka kwenye Lori hilo lililokuwa likitokea Ubungo kwenda bandarini na kusababisha foleni kubwa.

Picha kwa hisani ya East Africa Televishion Facebook Page unaweza kui Like kupata updates ya masuala mbalimbali yanayoendelea kila siku.

No comments:

Post a Comment