Serikali inapanga kupanua usafiri wa reli jijini Dar es Salaam kwa kujenga reli nyingine mpya katika mwaka wa fedhaa 2013/2014.
Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe, amesema wizara yake kwa kushirikiana na kampuni simamizi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) imepanga kujenga reli mpya itakayopita Luguruni, Bunju, Chamazi na Pugu.
Waziri Mwakyembe amesema wizara yake kwa sasa inaangalia uwezekano wa wa kuanzisha huduma maalum ya kati ya stesheni na Gongo la Mboto ili kuhudumia abiria wanaoshuka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere.
Amesema hivi sasa serikali inafanya mchakato wa kumpata mwekezaji na mwendeshaji wa huduma ya usafiri wa treni ya abiria katika jiji la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment