HOME

May 21, 2013

RAIS BARRACK OBAMA KUITEMBELEA TANZANIA JUNE!!


Ikulu ya Marekani imesema kuwa rais wa nchi hiyo Barack Obama
atatembea nchi za Senegal, Afrika Kusini na Tanzania mwezi Juni
mwaka huu lakini hatafika Kenya.

Taarifa hiyo ya Ikulu haijasema kwanini rais Obama hataitembelea
Kenya lakini inaonekana anazingatia suala la rais  Uhuru Kenyatta na naibu rais wake William Ruto wanakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya ICC inaweza kuwa sababu.

Rais Obama anatarajia kukutana na wabunge ikiwa ni pamoja na
wafanyabiashara na viongozi wa taasisi za kiraia na vijana katika ziara yake.

No comments:

Post a Comment