HOME

May 31, 2013

TAZAMA ENEWZ KIKAO KUHUSU ALBERT MANGWAIR!!

Kamati ya kusimamia shughuli za Msiba wa msanii Albert Mangwea kwa hapa Tanzania, imeundwa jioni ya jana Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam, ikihusisha baadhi ya wasanii wadau na wanafamilia wa msanii huyu kwaajili ya kuhakikisha kuwa taratibu zote zinaenda sawa mpaka mwili wa marehemu unarudishwa nyumbani Tanzania kwa maziko.



Leo pia kwenye CHAT KIKAANGONI LIVE ni Kufuatia kifo cha msanii Albert Mangwair,Leo IJUMAA saa SITA KAMILI, EATV itatoa nafasi pekee kwa mashabiki wa Albert Mangwair wa Facebook kupitia page ya East Africa Television (EATV) kuzungumza yao ya moyoni kuhusu Ngwair, kuanzia alipoanza muziki na maisha yake kwa ujumla mpaka kifo kilipomfika!

May 29, 2013

PICHA: HALI ILIVYOKUWA LEADERS CLUB WASANII WALIPOKUTANA, KAMATI YAUNDWA!!

Ndugu, Jamaa na marafiki wa msanii Albert Mangwea wamekutana leo jioni kuanzia saa kumi jioni maeneo ya Leaders Club kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu msiba huo ikiwa ni kuangalia kwa pamoja kile wanachoweza kufanya kwa pamoja na taratibu nzima ikiwemo michango kuhusu msiba mzima. 

Kupitia Umoja wa wao, Wasanii hao wameweza kuunda kamati ambayo inaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni kaka wa Marehemu Kenneth Mangweha ambapo wengine waliomo katika kamati ni pamoja na Adam Juma, P Funk Majani, Mez B, Mchizi Mox, Rommy Jones, Noorah, Michelle, Lady Jay Dee, Prof Jay, J Mo, na Dj Choka ambaye atahusika na kuzungumza kupitia mitandao yani Facebook na Twitter ambapo kwa taarifa zote kutoka kwake zitakuwa zimethibitishwa na kamati hiyo.

Mwanamitindo Flaviana Matata, Sajjo na Mwana FA
Wana kamati wakijadiliana baada ya kupewa muda wa kujadili mambo machache kabla ya kuja na taarifa yao fupi waliyoitoa kupitia kwa wadau na vyombo vya habari.



Noorah, Mez B na Proffesa Jay

Dada wa Marehemu Liloti Mangweha akizungumza kwa uchungu na kuelezea mengi kuhusu mdogo wake ikiwemo jinsi alivyopokea taarifa na kusema alikuwa katika hali mbaya ambayo hataisahau kwani alikuwa ndani ya daladala na hakujua kilichotokea baada ya hapo.
Baba mzazi wa msanii Dully Syke akizungumza anavyomfahamu marehemu ambapo amesema atamkumbuka kuna nyimbo ilikuwa wafanye wote lakini ndio hivyo kazi ya Mungu haina makosa.
Kala Jeremiah amemwelezea Ngwea kama msanii wa pekee alikuwa 100% mkali wa Free Style na alimpenda kwa nyimbo kali kama Ghetto langu iliyom inspire kuingia kwenye Game.
Mwana FA amesema ni vitu vingi vya kukumbuka kutoka kwa Ngwea lakini kikubwa ni uwezo wake wa kuandika na mashairi yake kutojirudia hadi akatoa mfano kuwa mara nyingi alikuwa akimwambia Ngwea kwamba ana Range anatembea nalo kichwani lakini Ngwea alimjibu kuwa si Range moja tu bali mawili anamiliki kichwani kwake so tunaweza kuona jinsi gani alikuwa mtu muhimu kwenye game.
Adam Juma alichaguliwa kama mzungumzaji wa kamati hiyo ambapo ametoa taratibu zote watakazofanya wao kama kamati ambapo amesisistza watu kushirikiana kwani msiba ni wetu sote hakuna mwenye mamlaka ya kuhodhi bali ni makubalino ya familia ndio yataendesha shughuli nzima
P Funk majani nae amezungumza lakini alishindw kutokana na uchungu aliokuwa nao juu ya msiba kwani bado haamni kama Ngwea hayupo tena.

PICHA: HUZUNI KWA WASANII, CHEMBA SQUARD WAKIWA STUDIO EAST AFRICA RADIO!!

Wasanii wa karibu sana wa msanii Albert Mangwea waliofahamika kama Chemba Squad leo walipata nafasi ya kufika katika studio za East Africa Radio kumzungumzia kwa kifupi Marehemu ambapo walionekana kuwa na huzuni kubwa sana kumpoteza mwana kundi mwenzao.
Kushoto Dogo Hamidu ambaye alikuja kuzungumzia maisha ya wabongo nchini Afrika Kusini ambapo amezungumza mengi na kulia ni Mchizi Mox ambaye amekuwa busy kushughulikia taratibu nzima za msiba wa rafiki yake Ngwair ambapo amehamasisha wadau kukutana leo saa 10 jioni pande za Leaders Club ili kuzungumza kuhusu msiba huo
Noorah pamoja na Mez B wakiwa ndani ya studio
Mchizi Mox
Mez B akiwa katika majonzi ambaye hapo alipo anaumwa lakini amejitahidi ili kuja kutoa salamu zake za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Albert Mangwea.
Watangazaji wa kipindi cha Power Jams Sam Misago na Ana Peter wakiwa kwenye show
Mchizi Mox akimzungumzia marehemu na historia yao kwa ufupi jinsi walivyokutana na marehemu pamoja na taratibu za msiba kwa ufupi.

DJ Kim

UPDATES: TAARIFA ZA MAZISHI YA MAREHEMU ALBERT MANGWEA!!

Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangweha ambaye yuko Mbinga Songea kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani baba mkubwa wa Ngwair, David Mangweha ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi Beach. Ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini baba huyo mdogo amesema wanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa.

Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na kaka yake yaani baba mkubwa wa marehemu. Kuhusu mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Afrika Kusini baba mdogo amesema kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili huo utafika hapa lakini kuna ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na ubalozi wa Afrika Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa.

Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho baba mdogo na baba mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifa.

May 28, 2013

ALBERT MANGWEA IS NO MORE!


Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa mwanamuziki wa Hip-Hop wa Tanzania Albert Mangwea amefariki dunia huko Afrika Kusini alipokwenda akiwa na Suma Lee. Taarifa zinasema kuwa rafiki wa karibu wa wasanii hao alitoa taarifa baada ya Ngwair kutoamka tangu alipolala jana. Inasemekana kuwa Ngwea amefariki kutokana na over-dose. Ngwea alitangazwa kufariki baada ya kufikishwa katika hospitali ya Hellena Joseph.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU ALBERT MANGWEA.

PICHA: OMBAOMBA ASHUSHIWA KICHAPO BAADA YA KUJIFANYA MLEMAVU!





















Mzee Mmoja ambaye amekuwa akiigiza ni mlemavu asiye na mguu mmoja na mkono mmoja ameambulia kichapo cha wananchi wenye hasira kali wa kijiji cha Miyomboni mjini Iringa.

Tapeli  huyo  mbali ya kuumbuliwa kwa kutakiwa kuonyesha miguu  yake yote pamoja na mikono yake yote bado amepata kuchezea  kichapo kiasi cha kunusurika kuuwawa na wananchi hao wenye hasira kali.

Tukio la mzee huyo kubainika kama ni tapeli kwa mara ya kwanza  mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com na www.matukiodaima.com ndio ulipata kufichua siri hiyo ya omba omba huyo kuwa si omba omba kutokana na kumnasa akijiweka mfano wa mlemavu .

Kutokana na kufichuliwa kwa siri hiyo ya kujiigiza kuwa ni omba omba mlemavu wananchi wamekuwa wakimtimua kila kona anayokaa tapeli huyo na kumtimua mbio kabla ya leo wananchi hao kuamua kumkimbiza kutoka eneo la Hazina Ndogo hadi Miyomboni na kuanza kumpa kichapo hadi alipoamua kuonyesha viungo vyote kuwa si mlemavu.

Tapeli huyo mbali ya kujifanya ni mlemavu wa viungo wakati mwingine huwa anajifanya ni mtu asiyeongea (bubu) asiye na viungo kama mikono na miguu ila wakati mwingine akijifanya ni hana mguu mmoja na kuwaomba watu fedha za matibabu .




Kwa hisani ya http://iringa-yetu.blogspot.com

May 27, 2013

SHUHUDIA WILL SMITH AKIPIGA PENALTY KWENYE SHEREHE ZA FAINALI YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE.

Kuelekea fainali ya UEFA Champions League iliyopigwa juzi na Bayern Munich kuukwaa uchampion wa Ulaya, staa wa Hollywood Will Smith na mwanae Jaden Smith walipata nafasi ya kushiriki the Ultimate Champions Match ambayo pia ilishirikisha wakali wa zamani kama Luis Figo, Gianfranco Zola na Robert Pires.


Isivyotegemewa na wengi, baba na mwana Smith walijikuta wakiiba show nzima kutokana na vimbwanga vyao katika uchezaji mpira hasa penalty.

Kati ya penalty KUMI walizopiga, walifanikiwa kumfunga goli moja tu, Edwin Van De Sar aliyekuwepo golini, baada ya Will Smith kuamua kumzuia asidake penalty hiyo.

Fuatilia video ya tukio hilo kwa ufupi hapa chini.

KUTANA NA WAWAKILISHI WA TANZANIA KATIKA JUMBA LA BIG BROTHER AFRICA SEASON 8 - THE CHASE


FEZA KESSY 
Soma wasifu wake wa BBA8 HAPA


AMMY NANDO
Soma wasifu wake wa BBA8 HAPA

BAADHI YA PICHA ZA AJALI YA TRENI NA GARI AINA YA RAV 4 UKONGA ASUBUHI HII.




Taarifa zinasema kwamba kuna ajali imetokea leo asubuhi maeneo ya Ukonga, ambayo imehusisha treni na gari aina ya RAV 4 ambayo ndani ilikuwa na watu wawili. Dereva wa RAV 4 amekufa papo hapo na abiria ambaye ni mwanamke hali yake ni mbaya yupo mahututi hospitali!

Picha kwa hisani ya MPEKUZI BLOG.

NEYMAR KUJIUNGA NA BARCA MWEZI JULAI.


Staa wa Brazil na klabu ya Santos Neymar da Silva Santos Jr, hatimaye amekubali kujiunga na klabu yenye mafanikio makubwa ya Hispania, Barcelona. Ripoti zinaonesha kuwa Neymar, ataichezea klabu hiyo kuanzia Julai mwaka huu, mara baada ya kumalizika kwa kombe la mabara. Neymar amejitia kitanzi cha miaka mitano kwa miamba hiyo ya Ulaya yenye wakali kama Lionel Messi, Xavi Hernandez, Andre Iniesta na Pedro Rodriguez.

Hapa chini ni official Twitter handle ya Barca, ilipo-confirm habari hizi.