Mtandao mmoja wa habari nchini Brazil umechapisha habari kuwa mvulana mdogo wa miaka miwili ambaye alifariki dunia aliinuka na kukaa ndani ya jeneza kisha akaomba maji na baadae akalala tena katika jeneza akiwa hana uhai.
Habari hiyo ambayo sio rahisi mtu kuamini, mtandao huo wa ORM umedai kwamba mtoto huyo ambaye ametambulika kwa jina la Kelvin Santos alikuwa hapumui wakati akipatiwa tiba ya homa ya mapafu katika hospitali ya Belem, Kaskazini mwa Brazil Ijumaa iliyopita.
Lakini saa moja kabla ya mazishi ya mtoto huyo siku ya Jumamosi, mtoto huyo marehemu aliinuka na kukaa ndani ya jeneza na kusema kama anaweza kupata maji na familia iliahirisha mazishi kwa saa moja wakiwa na matumaini kuwa angeamka tena, lakini haikutokea na kuamua kumzika
saa kumi na moja jioni siku hiyo.
No comments:
Post a Comment