HOME

Jun 11, 2012

TAIFA STARS YAICHAPA GAMBIA 2 - 1!!

 Mchezaji wa timu ya taifa Taifa Stars Mrisho Ngasa akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Gambia The Scorpions wakati timu hizo zikichuana katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil, mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Timu ya soka ya Tanzania, Kili Taifa Stars, jana ilivuna ushindi wake wa kwanza katika hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014, nchini Brazil kwa kuifunga Gambia mabao 2-1.

Licha ya Stars kuanza kwa nguvu mechi hiyo kwa lengo la kushinda mbele ya mashabiki wake kupoza machungu ya kufungwa mechi ya kwanza, kwa mshangao wa wengi, dakika ya saba waliruhusu bao, likifungwa kwa kichwa na Momodou Ceesay kutokana na krosi ya Saihou Gassama.

Kipindi cha pili kilianza kwa ushindani mkubwa kwani wakati Stars ikisaka bao la kusawazisha, huku wakipoteza nafasi kadhaa za kufunga, Gambia walijitutumua kulinda huku wakishambulia kwa kushtukiza.

Dakika ya 60, Shomari Kapombe aliifungia Stars bao la kusawazisha kwa kichwa cha kuparaza, hivyo nderemo na vifijo vya mashabiki kuuhanikiza Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment