HOME

Jun 5, 2012

MBUNGE ALIYEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA!!



Pichani Mbunge wa jimbo la Bahi Tanzania, Bw. Omar Ahmed Badwel akiwa anafikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za rushwa.
  
Mbunge wa jimbo la Bahi nchini Tanzania, Bw. Omar Ahmed Badwel amepandishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka mawili ya kudai na kupokea rushwa.

Katika shitaka la kwanza, imedaiwa kuwa kati ya Mei 30 na Juni 2 mwaka huu, mtuhumiwa aliomba rushwa ya shilingi milioni nane kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Bi. Sipora Liana ili ashawishi kamati yake ipokee na kukubali ripoti ya hesabu za halmashauri hiyo.

Imedaiwa pia kuwa kipindi hicho hicho, mtuhumiwa amekamatwa akipokea rushwa ya shilingi za milioni moja za Tanzania, kutoka kwa Bi. Sipora kwa lengo lilelile la kushawishi kamati yake ipokee na kupitisha hesabu za halmashauri ya wilaya ya Mkuranga.

No comments:

Post a Comment