Watu wengine wawili wamekufa na kufanya idadi ya waliokufa katika
shambulio la bomu lililotokea Mombasa nchini Kenya siku ya Jumapili
kufikia watatu huku wengine 25 wakipatiwa matibabu katika hospitali ya
Jimbo la Pwani baada ya kujeruhiwa.
Tukio hilo ambalo limetokea saa nne kamili usiku limetokea katika baa moja wakati watu wakiangalia mechi ya mpira wa miguu.
Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema waliona wanaume wawili na mwanamke mmoja
wakiwasili ndani ya gari aina ya Rav 4 na kushuka kuelekea baa hiyo na
baadae mlipuko huo ulitokea na gari kutokomea.
Mlipuko huo umetokea saa chache baada ya serikali ya Marekani kutoa tahadhari ya ugaidi na kuonya raia wake kuwa waangalifu katika Pwani ya Kenya.
No comments:
Post a Comment