Huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya zimerejea katika hali ya kawaida baada ya kusitishwa kwa saa nane kuruka na kutua ndege katika uwanja huo baada ya hitilafu kutokea katika barabara ya kutua na kuruka katika uwanja huo.
Uwanja huo wenye shughuli nyingi ulifungwa saa kumi alfajiri ya leo baada ya ndege ya shirika la ndege la Egypt Air kuvutwa nje ya njia ya kutua ilipokuwa ikitua ikiwa na abiria 123 kutoka Cairo ambao wote walisalimika na kupelekwa katika jengo la uwanja huo.
Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata (KAA) imesema katika taarifa yake kuwa huduma katika uwanja huo zimerejea katika hali yake ya kawaida kuanzia saa sita mchana leo baada ya kutokea hitilafu katika barabara ya kuruka na kutua.
No comments:
Post a Comment