Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Bernad Membe |
Kauli hiyo imetolewa bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Bernad Membe wakati akijibu swali la mbunge wa Konde Mh. Khatib Said Haji aliyetaka kujua serikali imejipanga vipi kukabiliana na janga la nchi wahisani watakapotoa misaada yao kwa lengo la kushinikiza ndoa za jinsia moja.
Akijibu swali hilo Mh. Membe amesema dini zote hapa nchini hazikubaliani na uwepo wa ndoa ya jinsia moja na viongozi wake wapo mstari wa mbele kukemea jambo hili na kwa maana hiyo utamaduni wa nchi na sheria za dini hazitambui ndoa ya jinsia moja.
No comments:
Post a Comment