HOME

Jun 30, 2012

SHUHUDIA INAVYOKUWA KWENYE DANCE 100% YA EATV!!

Dj Summer kutoka EA RADIO na EATV


Mchakato wa kusaka makundi bora ya ku-dance jijini Dar es Salaam unaofahamika kama Dance 100% umeweza kuvutia umati mkubwa uliojitokeza kushiriki na kushuhudia michuano mikali ambayo imefanikisha kupatikana na makundi 17 yaliyoonekana kufikia kiwango kilichorodhisha waamuzi.

Mpango mzima wa Dance Miamia ulianza kwa kasi kubwa ndani ya viwanja vya Leaders Club Kinondoni, na kufuatiwa na uwanja wa Don Bosco Wilayani Ilala na kuishia Wilaya ya Temeke ndani ya uwanja wa TCC Changombe.
Majaji wa mashindano hayo ni wakali wenye experience Lotus Kyamba kutoka EATV ambaye alianza kudance tangu akiwa na umri wa miaka mitano,Super Nyamwela wa Extra Bongo mwenye Experience ya kutosha pamoja na mkali Prince Dully Sykes.

Utaratibu wa kutoa marks ulikuwa kama hivyo kwa kutumia vibao vyenye asilimia 10 mpaka 100 kama shindano linavyosema.



Usikose kuangalia show hii kali ya Dance Mia Mia kila Jumatano saa 3 na nusu usiku ili ujionee mwenyewe kilivyosanuka kuanzia pale viwanja vya Leaders Club Kinondoni,Ilala na baadae Don Bosco Jijini Dar es Salaam, kupitia EATV Pekee!!!

Jun 25, 2012

WATU WATATU WAMEKUFA KATIKA SHAMBULIO LA BOMU MOMBASA!!

Watu wengine wawili wamekufa na kufanya idadi ya waliokufa katika shambulio la bomu lililotokea Mombasa nchini Kenya siku ya Jumapili kufikia watatu huku wengine 25 wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Jimbo la Pwani baada ya kujeruhiwa.


Tukio hilo ambalo limetokea saa nne kamili usiku limetokea katika baa moja wakati watu wakiangalia mechi ya mpira wa miguu.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema waliona wanaume wawili na mwanamke mmoja wakiwasili ndani ya gari aina ya Rav 4 na kushuka kuelekea baa hiyo na baadae mlipuko huo ulitokea na gari kutokomea.

Mlipuko huo umetokea saa chache baada ya serikali ya Marekani kutoa tahadhari ya ugaidi na kuonya raia wake kuwa waangalifu katika Pwani ya Kenya.

Jun 20, 2012

TANZANIA KUTORIDHIA MISAADA YA MASHARTI KUHALALISHA USHOGA!!

Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Bernad Membe
Serikali ya Tanzania imesema iko tayari  kujifunga mikanda na kujibeba yenyewe kuhakisha haikubali kudhalilishwa kiutu na utamaduni wake kwa kukubali kupokea misaada ya masharti itakayotulazimisha kukubaliana na  ndoa za jinsia moja. 

Kauli hiyo imetolewa bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Bernad Membe wakati akijibu swali la mbunge wa Konde Mh. Khatib Said Haji aliyetaka kujua serikali imejipanga vipi kukabiliana na   janga la nchi wahisani watakapotoa misaada  yao kwa lengo la kushinikiza ndoa  za jinsia moja.

Akijibu swali hilo Mh. Membe amesema dini zote  hapa nchini hazikubaliani  na uwepo wa ndoa ya jinsia  moja  na viongozi wake wapo mstari wa mbele kukemea  jambo hili na kwa maana hiyo utamaduni wa  nchi  na  sheria za dini hazitambui ndoa ya jinsia moja.

WEMA KUMLETA OMOTOLA JALADE KUZINDUA SUPASTAR!!

Ni onyesho maalum la familia
Mkali wa filamu nchini Nigeria na Afrika, Omotola Jalade atazindua filamu ya Wema Sepetu Jumapili hii katika Ukumbi wa Hoteli ya Girafee Ocean View, iliyopo Mbezi Beach.


Filamu hiyo iitwayo Super Star imechezwa na Wema, ikionyesha maisha ya mtu maarufu na changamoto anazozipata ikiwemo kuandikwa  mambo mbalimbali ikiwemo taarifa za vyombo vya habari.
Katika uzinduzi huo, bendi kutoka Tanzania House Of Talent (THT) watatoa burudani, kabla ya mashabiki kupata nafasi ya kupiga picha na msanii huyo.


Omotola, ambaye ni mke wa rubani Kapteni Matthew Ekeinde, ambao walifunga ndoa yao angani kwenye ndege atatoa nafasi ya kupiga picha na watu kadhaa.


Katika uzinduzi huo, pamoja na burudani ya muziki, mashabiki watakaofika hapo, watapata pia fursa ya kuiona filamu ya Super Star katika viwanja hivyo vya hoteli hiyo iliyoko ufukweni.


Omotola ambaye yuko kwenye ndoa kwa miaka 16 akiwa na watoto wanne, ana jumla ya albamu mbili za muziki.


Msanii huyo ambaye mwaka jana alitangaza kuachana na kucheza filamu kutokana na kuandikwa vibaya, anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwenye uzinduzi huo ambao kiingilio kitakuwa Sh 30, 000 kwa wakubwa na watoto 10,000.

SUPER NYAMWELA AOA KINYEMELA!!

Super Nyamwela
Mnenguaji na mwanamuziki mahiri wa bendi ya muziki wa dansi nchini Tanzania ya Extra Bongo Next Level Wazee wa Kizigo, Super Nyamwela hatimae amevuta jiko lake la pili na safari hii ameamua kufanya siri.

Ndoa hiyo imefungwa kwa siri ambapo baadhi ya watu wameshangaa kutoalikwa kwenye sherehe ya ndoa hiyo iliyofungwa juzi Jijini DSM.

Hivi karibuni mnenguaji huyo aliwahi kufunguka kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa na East Africa Tv kuwa baada ya aliyekuwa mke wake kufariki miaka kadhaa iliyopita anatarajia kufunga pingu za maisha na mpenzi wake ili waweze kumlea mtoto wake.

Jun 12, 2012

NAVIO - ONE & ONLY - HOT NEW SINGLE!!


Brand new audio release from Navio called "One & Only". A catchy African Hip Hop and RnB fusion project produced by Aethan and Samurae at Talent Africa music studios.  The chorus of the song features the talented young vocalists Richy and Martha from the Talent Africa music label.  One & Only is the flagship single of Navio's upcoming album which will be released in October 2012.

The highly anticipated video for One & Only will be released worldwide on June 13th, 2012. Navio flew all the way to Durban, South Africa to shoot this adventurous and thrilling video in which scenes consist of him performing numerous extreme activities such as Quad Biking, Shark Diving and Bungee Jumping off a cliff.  This is the highest budget video ever shot by an East African Artist and is sure to raise the bar across the region.

View the trailer for One & Only video by clicking the link below:
http://www.youtube.com/watch?v=dbL4wwihCYw

Follow Navio on Facebook and Twitter:
Facebook: Navio
Twitter: @naviomusic
Webiste: www.naviomusic.com

For bookings, artist info, interviews, or any other information please reach us on the contact details listed below.

---
PR and Communications Department
Talent Africa Group
Mobile - +256 767 581 695
Email: info@talentafricagroup.com
Facebook: Talent Africa
Twitter: @talentafrica

"East Africa's leading 360 Entertainment Company"

PSQUARE KUTOKA NAIJA WAACHIA VIDEO MPYA FEAT RICK ROSS "BEAUTIFUL ONYINYE"!!

 
Kuiona Bonyeza Link hapo chini
http://www.youtube.com/watch?v=lY2H2ZP56K4

Jun 11, 2012

LEWIS HAMILTON ASHEREKEA USHINDI KWA STYLE YA AINA YAKE!!

Hamilton alijirusha kinyume nyume kwenye bwawa la kuogelea ikiwa ni staili ya kusherekea ushindi

Dereva wa McLaren Lewis Hamilton jana aliibuka mshindi wa mpambano wa Canadian Grand Prix na michuano hiyo ya mwaka huu imekuwa ikimpata mshindi tofauti tangu ilipoanza msimu huu.

Hamilton alipambana kutoka nafasi ya tatu na kuwapita Fernando Alonso na Sebastian Vettel katika mizunguko ya mwisho ya mpambano huo.

Mkakati wa Alonso kusimama mara moja haukumsaidia na kujikuta akiporomoka kutoka kileleni na kumaliza akiwa wa tano baada magurudumu ya gari lake kuonyesha dalili za kutostahimili.

AFRIKA MASHARIKI YATAKIWA KUIMARISHA USALAMA!!

Wakuu wa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Na Mwandishi wa EANA

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, Dk. Julius Rotich amesema kanda hiyo inahitaji mkakati madhubuti na unaoweza kutekelezeka ili kupambana na changamoto za vitisho vya usalama.

''Tunakiwa tujiweke tayari kimkakati kwa kuzingatia vitisho vya kiusalama kama vile kwenye bahari,uharamia,biashara ya fedha,ugaidi na uhalifu wa kwenye mitandao ikiwa ni miongoni mwa vitisho vilivyopo, kwa lengo la kuhakikisha kwamba amani na utulivu vinabaki kuwa  vipaumbele katika nchi za Afrika Mashariki,'' alisema.

Dk. Rotich alisema hayo alipokuwa anafungua mkutano wa siku tano wa watasalamu wa EAC kutathmini mkakati wake wa Amani na Usalama, mjini Dar es Salaam, Tanzania, Alhamisi.

Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Ofisa wa Amani na Usalama wa EAC, Didacus Kaguta, Naibu Katibu Mkuu huyo alisisitiza kuzingatia na kuendeleza masuala ya amani na utulivu ambayo ni nguzo muhimu katika agenda ya mtangamano wa EAC.

Mkataba wa EAC unatambua amani na usalama kuwa ni masuala muhimu ya awali kabisa kufanikisha mtangamano huo ambao ni muhimu zaidi kwa sasa wakati kanda inaelekea katika  majadiliano ya muungano wa fedha.

Muungano wa fedha ni hatua ya tatu ya mtangamano wa EAC ikiwa imetanguliwa na Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja.

Naye Mwenyekiti wa kikao hicho David Njoka alisema kanda hiyo ya EAC haiwezi kukaa kimya bila kushughulikia vitisho vipya vya usalama ambavyo vinaweza kuvuruga lengo la kuwa na Afrika Mashariki iliyoungana na yenye mafanikio.

Mkutano huo uliohudhuriwa na wataalamu kutoka jeshi, polisi,usalama,magereza,mahakama na sekta ya sharia,uliratibiwa na EAC.

LIBYA KUFANYA UCHAGUZI MWEZI JULAI!!

Mkuu wa tume ya uchaguzi Bw. Nuri al Abbar
Maafisa nchini Libya wamesema kuwa mapigano kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa kikabila kusini mwa mji wa Kufra nchini humo yameendelea kwa siku ya pili.

Takribani watu 16 wameuwawa tangu kuanzia kwa mapigano hayo siku ya Jumamosi huku wanawake na watoto wakiwa kati ya waliowawa.

Serikali ya Libya imekuwa katika jitihada za kudumisha ulinzi tangu kuondolewa madarakani kwa kanali Muammar Gaddafi mwaka jana.

TAIFA STARS YAICHAPA GAMBIA 2 - 1!!

 Mchezaji wa timu ya taifa Taifa Stars Mrisho Ngasa akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Gambia The Scorpions wakati timu hizo zikichuana katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil, mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Timu ya soka ya Tanzania, Kili Taifa Stars, jana ilivuna ushindi wake wa kwanza katika hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014, nchini Brazil kwa kuifunga Gambia mabao 2-1.

Licha ya Stars kuanza kwa nguvu mechi hiyo kwa lengo la kushinda mbele ya mashabiki wake kupoza machungu ya kufungwa mechi ya kwanza, kwa mshangao wa wengi, dakika ya saba waliruhusu bao, likifungwa kwa kichwa na Momodou Ceesay kutokana na krosi ya Saihou Gassama.

Kipindi cha pili kilianza kwa ushindani mkubwa kwani wakati Stars ikisaka bao la kusawazisha, huku wakipoteza nafasi kadhaa za kufunga, Gambia walijitutumua kulinda huku wakishambulia kwa kushtukiza.

Dakika ya 60, Shomari Kapombe aliifungia Stars bao la kusawazisha kwa kichwa cha kuparaza, hivyo nderemo na vifijo vya mashabiki kuuhanikiza Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

KENYA KATIKA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO!!

Prof George Saitoti enzi za uhai wake
Kenya imetangaza siku tatu za maombolezo baada ya kifo cha Waziri wa Usalama wa Kenya, Prof. George Saitoti na naibu wake, Orwa Ojode, kwenye ajali ya helikopta ya polisi katika eneo la Ngong, nje ya Nairobi.

Ajali ya helikopta iliyochukua maisha ya wakenya sita akiwemo waziri wa usalama wa ndani wa Kenya Prof. George Saitoti na naibu wake Orwa Ojode jana asubuhi.
 
Wakati huo huo rais Mwai Kibaki wa Kenya leo asubuhi ameongoza kikao cha baraza la mawaziri kujadili vifo hivyo.


Sababu ya ajali hiyo haijafahamika ingawa mashuhuda wamekuwa wakielezea jinsi walivyoiona helikopta hiyo ikitoa moshi na kupotea uelekeo.

Jun 8, 2012

GAMBIA YATUA KUIKABILI STARS!!

Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) imewasili nchini jana (Juni 7 mwaka huu) saa 5.30 usiku kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Msafara wa timu hiyo wenye watu 31 wakiwemo wachezaji 22 unaongozwa na
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Michezo wan chi hiyo, Malang Jassey.


Viongozi wengine ni Ofisa Utawala wa timu Modou Sowe, Kocha Luciano Machini, makocha wasaidizi Peter Bonu Johnson na Lamin Sambou, Kocha wa makipa Alhagie Marong, mtaalamu wa tiba mbadala (physiotherapist) Pa Matarr Ndow, Mtunza vifaa Sanna Bojang na Daktari wa timu Kalifa Manneh.


Wachezaji ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay, Demba Savage, Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.


Gambia ‘The Scorpions’ itafanya mazoezi yake ya kwanza leo (Juni 8 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume wakati kesho muda huo huo itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa.

HAKUNA ONGEZEKO LA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA UGANDA!!

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema kuwa hakutakuwa na nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma na wanasiasa wakati akilihutubia taifa jana.


Katika hotuba hiyo rais Museveni aliainisha matatizo ambayo taifa hilo linakabiliana nayo ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha kwa ajili ya kuendeleza miundo mbinu na kuainisha kuwa nyongeza ya mishahara sio
kipaumbele.


Katika hotuba yake rais amesema nchi hiyo itakusanya fedha kwa ajili ya kujenga barabara za lami 44 ambazo zimeainishwa na UNRA kwa kuziimarisha katika mwaka ujao wa fedha.

JACKIE LANDS SISQO GIG!!

Jackie Chandiru’s star is certainly on the rise and she isnt ready to let matters of the heart get in the way of her career.


After blowing away fans at the Miss Uganda concert with her impressive rendition of the National anthem last Friday latest news filtering in will certainly put a smile on her face.


Jackie has been chosen the last and  curtain-raising Ugandan act for the Sisqo concert and Dr. Jose Chameleone and Ghetto President Bobi Wine.


THANKS:NEW VISION UGANDA

Jun 7, 2012

BASATA YATOA SOMO KWA WAANDAAJI EPIC BSS!!

Mkurugenzi wa Benchmark Production Ritha Paulsen akizungumza katika semina hiyo.
Kutoka kushoto Mratibu wa matukio wa Basata Malimi Mashili,majaji wa EPBSS wakiongozwa na Madam Ritha,Master J,na Salama Jabir.
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limeendesha semina ya siku moja kwa majaji wa shindano la Epic Bongo Star Search 2012 kwa kuwataka kuzingatia maadili ya kazi zao.

Akitoa somo kwa majaji hao mratibu wa matukio wa Basata Malimi Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa asilimia kubwa  ya washiriki wanategemea zaidi msaada wao katika kukuza vipaji.

Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa mazingira waliyotoka washiriki na kuangalia namna ya kuwasaidia kulingana na mikoa yao kwa kuwa wapo ambao wana vipaji lakini wanatatizwa na suala la kuyazoea mazingira.

Alisema kuwa kwa kuwa mwaka huu EBSS itaruhusu washiriki wa miaka 16 hivyo ni vema zaidi wakazingatia suala la sauti kulingana na umri wa mshiriki sababu watakuwepo wenye sauti za kitoto pia.

Pia aliwataka majaji hao kuhakikisha kuwa hawatoi aina yoyote ya upendeleo na wala kuwa karibu zaidi na baadhi ya washiriki wa shindano hilo.

Pia alisisitiza kuwa majaji wanalo jukumu kubwa la kuwaelekeza namna ya kuimba, kuvaa, kujiheshimu na usafi wa mwili pia.

“Hii ni semina ya kuwekana sawa tu kwa kuwa hili shindano lipo kwa muda mrefu na majaji mmekuwa mkifanya vema, kwa niaba ya BASATA napenda kuchukua muda huu kuwataka muwe makini katika kuzingatia maadili haya niliyoyasema na hata mengine pia”alisema Mashili.

Naye Mkurugenzi wa Benchmark Production inayoandaa shindano hilo Ritha Paulsen alisema kuwa semina hiyo ni muhimu kwa majaji kwa kuwa  muda mzuri wa kukumbushana mambo muhimu yahusuyo muziki.

Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 16 katika ukumbi wa Royal Village.

Majaji wa shindano hilo waliohudhuria ni pamoja na Jaji Mkuu Ritha Paulsen, Master Jay, Salama  pamoja na mratibu wa EBSS kutoka Basata Vicky Temu.

MTOTO ALIYEFUFUKA AKAOMBA MAJI KISHA AKAFA TENA!!

Mtandao mmoja wa habari nchini Brazil umechapisha habari kuwa mvulana mdogo wa miaka miwili ambaye alifariki dunia aliinuka na kukaa ndani ya jeneza kisha akaomba maji na baadae  akalala tena katika jeneza akiwa hana uhai.


Habari hiyo ambayo sio rahisi mtu kuamini, mtandao huo wa ORM umedai kwamba mtoto huyo ambaye ametambulika kwa jina la Kelvin Santos alikuwa hapumui wakati akipatiwa tiba ya homa ya mapafu katika hospitali ya Belem, Kaskazini mwa Brazil Ijumaa iliyopita.


Lakini saa moja kabla ya mazishi ya mtoto huyo siku ya Jumamosi, mtoto huyo marehemu aliinuka na kukaa ndani ya jeneza na kusema kama anaweza kupata maji na familia iliahirisha mazishi kwa saa moja wakiwa na matumaini kuwa angeamka tena, lakini haikutokea na kuamua kumzika
saa kumi na moja jioni siku hiyo.

Jun 6, 2012

BOMU LA KUJITOA MHANGA LAUA 21 AFGHAN!!

Polisi nchini Afghan imeviambia vyombo vya habari kuwa bomu la kujitoa mhanga limeua watu 21 katika shambulio lililofanyika katika hoteli karibu na mji wa Kandahar.


Mkuu wa polisi wa jimbo hilo Abdul Raziq amesema madereva wanaowahudumia majeshi ya NATO walikuwa wanakusanyika katika hoteli hiyo wakati wa shambulio hilo.


Taarifa hiyo ya jeshi la polisi inasema watu 22 walijeruhiwa kufuatia shambulio hilo karibu na uwanja wa ndege wa mji huo.

SARAHA ADONDOKA NA JAMBAZI!!

 
Msanii wa kike aliyeweza kujichanganya vizuri na baadhi ya wasanii wa miondoko ya bongo flava nchini Tanzani, Saraha anayetokea nchini Sweden aendeleza cheche zake kwa kutoa vibao mbalimbali katika gemu hii ya muziki.


Akiwa anatamba na vibao kama Tanesco, Malaika na vinginevyo hivi sasa Saraha amefyatua audio track yake mpya aliyoipa jina 'Jambazi' iliyotayarishwa na mumewe Fundi Samweli katika studio ya Usanii Production.


Isikilize ngoma hapa!!

UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATTA WAFUNGULIWA!!


 Huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya zimerejea katika hali ya kawaida baada ya kusitishwa kwa saa nane kuruka na kutua ndege katika uwanja huo baada ya hitilafu kutokea katika barabara ya kutua na kuruka katika uwanja huo.

Uwanja huo wenye shughuli nyingi ulifungwa saa kumi alfajiri ya leo baada ya ndege ya shirika la ndege la Egypt Air kuvutwa nje ya njia ya kutua ilipokuwa ikitua ikiwa na abiria 123 kutoka Cairo ambao wote walisalimika na kupelekwa katika jengo la uwanja huo.

Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata (KAA) imesema katika taarifa yake kuwa huduma katika uwanja huo zimerejea katika hali yake ya kawaida kuanzia saa sita mchana leo baada ya kutokea hitilafu katika barabara ya kuruka na kutua.

VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

Mwaka 2011/2012 Kambi ya Upinzani Bungeni ilitangaza Vipaumbele vyake katika Bajeti Mbadala ambavyo vilikuwa:
1.    Kupunguza misamaha ya kodi mpaka 1% ya pato la Taifa kutoka 3%


2.    Kupunguza kodi kwenye bidhaa za mafuta ya petrol na dizeli ili kupunguza mfumuko wa bei
3.    Kufuta mfumo wa posho za vikao (Sitting allowances).
4.     Kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills Development levy-SDL) kwenye bodi ya mikopo ya  elimu ya juu.
Masuala haya pamoja na mengine yalikuwa sehemu ya Bajeti kivuli iliyowasilishwa Bungeni na Kambi ya Upinzani.
Mapendekezo mawili,
(1) Kodi za mafuta ya Petrol na Diseli na
(2) Tozo ya SDL yalikubaliwa na kutekelezwa. Pendekezo la misamaha ya kodi lilikubaliwa  lakini Serikali imeshindwa kulitekeleza na pendekezo la kufutilia mbali posho za vikao halikukubaliwa.
Kambi Rasmi ya Upinzani inataka maelezo ya kina ya kwa nini Serikali imeshindwa kutekeleza ahadi yake iliyoitoa Bungeni kwamba misamaha ya kodi itapungizwa mpaka kufikia 1% ya pato la Taifa. Halikadhalika Kambi ya Upinzani inarejea wito wake wa
kufutwa kwa Mfumo wa posho za vikao (sitting allowances).

Serikali imependekeza Bajeti ya Tshs. 15trillioni kutoka Tshs. 13 trillion. Hata hivyo ni dhahiri kwamba Bajeti ya 2011/12 ilikuwa ina changamoto kubwa za utekelezaji. Serikali ieleze itawezaje kutekeleza Bajeti ya 15trillioni?
Katika Bajeti Mbadala ya 2012/2013 Kambi ya Upinzani itajikita katika maeneo yafuatayo na kuishinikiza Serikali kuyatekeleza.
1. Kuendelea kushinikiza kupunguzwa kwa misamaha ya kodi mpaka 1% ya Pato la Taifa.
Hivi sasa misamaha ya kodi ni sawa na misaada yote kutoka nchi wahisani, Tshs 1.03 trillioni ni sawa na 3% ya Pato la Taifa.
2. Kuelekeza raslimali fedha kwenye maendeleo vijijini hasa kujenga miundombinu kama barabara za vijijini na umeme vijijini.
3. Kuelekeza fedha za kutosha  kukarabati Reli ya Kati na kufufua njia za Reli za Tanga, Moshi na Arusha.
4. Kuongeza wigo wa kutoza  tozo la ujuzi (Skills Development Levy) ambapo sasa waajiri wote walipe ikiwemo Serikali na mashirika ya umma. Pia kupunguza tozo hili mpaka 4% ambapo 1/3 itaenda VETA na vyuo vya Ufundi na 2/3 itaenda Bodi ya Mikopo
ili kukabili changamoto ya mikopo kwa wanafunzi.
5. Kushusha kima cha chini cha kodi ya mapato (PAYE) mpaka 9% ili kuwezesha wananchi wa hali ya chini kubaki na fedha za kutumia na kukuza uchumi.
6. Kuongeza mapato ya ndani na kupunguza mikopo ya kibiashara kwa kuhakikisha mapato ya ndani yanafikia 20% ya pato la taifa, kuongeza nguvu za kisheria na udhibiti ili TRA ikusanye mapato zaidi kwenye kampuni za simu na kwenye shughuli za uchimbaji wa
madini, mafuta na gesi.
7. Kutayarisha Taifa kuwa na uchumi wa Gesi.
8. Kupunguza /kufuta kodi kwenye bidhaaa za vyakula kwa muda maalum ili kushusha mfumuko wa bei.
9. Kuweka mfumo mpya wa elimu kwa kushirikisha sekta binafsi katika kutoa elimu kwa ubora zaidi, ikiwemo kuundwa kwa chombo cha Udhibiti wa Elimu(Regulatory authority)
10. Kutoa vipaumbele na unafuu vya kikodi kwa viwanda vya ndani vinavyotumia malighafi za nchni hasa za kilimo na zenye kuongeza ajira kama Korosho,Pamba na Mkonge.
Kambi ya Upinzani itaendelea kufuatilia kwa karibu sana suala la kukua kwa deni la Taifa amabalo limefikia hadi Tshs 22 trillioni na kutaka ukaguzi maalum kuhusu akaunti ya Deni la Taifa.
Kambi ya Upinzani itawekeza kusimamia kwa karibu suala la matumizi yasiyo na tija ya Serikali hasa kwenye  magari na posho mbalimbali na Kwamba  fedha nyingi zitumike kwa miradi  mikubwa ya maendeleo ili kukuza ajira. Halikadhalika namna ya kupta fedha za kutekeleza mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano


Asanteni sana!
…………………………….
Zuberi Kabwe Zitto(Mb)
Waziri Kivuli-Fedha na Uchumi.

FIRST LADY,PATIENCE JONATHAN RESPONDS TO ALLEGATIONS OF BEING RESPONSIBLE FOR DANA PLANE CRASH!!

The First Lady of Nigeria, Patience Jonathan came under criticism yesterday as news of the alleged closure of the nation’s airspace for a Presidential jet conveying her to Lagos on Sunday went viral on BlackBerry Messenger and online social networks.


The closure was said to have prevented the pilot of the distressed Dana Air’s plane from making an emergency landing at the airport. Reports circulated claimed that although the Dana plane had an engine failure, the distressed aircraft could have made it to the airport if it was not delayed by the VIP movement.


However, in response to this, the Special Assistant (Media) to the Minister of Aviation, Mr. Joe Obi, said the airspace was never closed for the First Lady on Sunday. He noted that the First Lady arrived in Lagos at about 4.45pm on Saturday, 2nd June, 2012 and only departed for Abuja on Monday, the 4th of June, 2012 at 1.30pm, whereas the ill-fated Dana flight 0992 departed Abuja on Sunday, 3rd of June, 2012 at 2.54pm and its last contact with the Lagos Control Tower was at 3.42pm as has already been announced.


The rumours prompted a response from the Office of the First Lady:


I am responding to the rumor mongers because of the involvement of the script writers of those that wish to heat up the polity of Nigeria at every event or given opportunity. Like they have always done, using every opportunity to make Nigeria ungovernable. Why would a group of people in different disguises want to play politics with this sad event just to get back to political rivals or superiors?


This morning, reports from one Ade Atobatele….Information Technology and Services has filtered the air. Don’t know which of the firms that is, claimed that the Dana Airline misfortune was caused by the closure of airspace for the first lady’s aircraft. He was quoted as saying he was informed by a pilot of a private Jet that also had to hover in the air for 2 hours 15mins before the airspace opened for landing. He has conned his story that the social, electronic and print media has started reporting it without verifying his source.

Jun 5, 2012

MBUNGE ALIYEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA!!



Pichani Mbunge wa jimbo la Bahi Tanzania, Bw. Omar Ahmed Badwel akiwa anafikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za rushwa.
  
Mbunge wa jimbo la Bahi nchini Tanzania, Bw. Omar Ahmed Badwel amepandishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka mawili ya kudai na kupokea rushwa.

Katika shitaka la kwanza, imedaiwa kuwa kati ya Mei 30 na Juni 2 mwaka huu, mtuhumiwa aliomba rushwa ya shilingi milioni nane kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Bi. Sipora Liana ili ashawishi kamati yake ipokee na kukubali ripoti ya hesabu za halmashauri hiyo.

Imedaiwa pia kuwa kipindi hicho hicho, mtuhumiwa amekamatwa akipokea rushwa ya shilingi za milioni moja za Tanzania, kutoka kwa Bi. Sipora kwa lengo lilelile la kushawishi kamati yake ipokee na kupitisha hesabu za halmashauri ya wilaya ya Mkuranga.

Jun 4, 2012

AJALI YAUA WATU 150 NIGERIA!!

Siku tatu za maombolezo ya kitaifa zimetangazwa kuanzia leo nchini Nigeria kufuatia ajali ya ndege ambapo zaidi ya 150 walikufa.


Ndege hiyo aina ya Boeing MD-83 iliangukia eneo moja la kuchapisha karatasi na makaazi mjini Lagos kabla ya kulipuka. Makundi ya wokozi yamekuwa eneo la ajali usiku kucha.


Taarifa zinasema abiria wote katika ndege hiyo walikufa. Hakuna majeruhi katika eneo la ajali japo haijabainika rasmi ni watu wangapi ambao wamekufa.


Ndege hiyo inamilikiwa na kampuni ya Dana Air ambayo hutoa huduma zake kati ya mji wa Abuja na Lagos. Ajali hiyo ilitokea katika mji wa Iju Kaskazini mwa uwanja wa ndege.