HOME

Apr 25, 2013

WANAUME WAGUMU KUPIMA UKIMWI!!

Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini Tanzania TACAIDS, imetoa tathmini ya mwitikio wa udhibiti wa Ukimwi, tathmini inayoonyesha kuwa idadi kubwa ya wanaume hawana tabia ya kwenda kupima mara kwa mara ili kubaini kama wamembukizwa au hawajaambukizwa virusi vya ugonjwa huo.

Mwenyekiti mtendaji wa tume hiyo Dk Fatma Mrisho ametaka kuwepo kwa mbinu za kuwashawishi wanaume kujenga tabia ya kupima na kufahamu afya zao ikiwemo afya ya uzazi.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo, Dk Mrisho amebainisha kuwa utafiti alioufanya kwa takribani miaka 10 unaonyesha kuwa asilimia 67 ya wanouguza waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi ni wanawake.

NOMINEES WA KILI AWARDS WATANGAZWA.....OMMY DIMPOZ, BEN POL WANG'ARA!!

Majina ya wasanii wa muziki Tanzania ambao wameweza kuingia katika kinyang'anyiro cha tuzo za muziki za Kilimanjaro, yametangtazwa leo rasmi jijini Dar es Salaam ili kuanza mchakato wa kupata washindi wa tuzo hizo kwa mwaka huu wa 2013.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe amesema Academy ilikaa mwishoni mwa wiki iliyopita na kufanya kazi nzuri ya kuchagua wasanii wa muziki waliofanya vizuri na kazi zao kupendwa na kukukbalika na wengi mwaka 2007.
Katika mchakato wa mwaka huu na kama hatua moja ya maboresho yake, Vipengelea ambavyo vitakuwa vikishindaniwa mwaka huu vimeongezeka na kufikia 35.

Wasanii ambao wameweza kung'ara kwa kutokelezea katika vipengele vingi ni pamoja na Ommy Dimpoz ambaye anatokelezea mara 7 katika categories 6, Ben Pol ambaye anatokelezea mara 6 katika categories 7, Kala Jeremiah na Fid Q katika categories 4 na wengineo.Mkuu wa Idara ya Mfuko na Uwezeshaji kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Angelo Luhala akizungumza machache katika zoezi la kutaja majina hayo.

Tuzo za Kilimanjaro Music zitafanyika kwa mwaka huu tarehe 8 Mwezi Juni katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, na katika kipindi hiki cha kati hatua zitakazofuata ni pamoja na Semina kwa wasanii na Upigaji kura ambao utaanza Mei tarehe 2.

Tuzo hizo zimeletwa na kampuni ya bia ya Tanzania kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la sanaa Tanzania BASATA.

PICHA ZA KATE ZAZUA UTATA...WAWILI WACHUNGUZWA!!

Mkuu wa uchapishaji wa gazeti la Ufaransa Closer na mmoja wa wapiga picha wanafanyiwa uchunguzi nchini Ufaransa kufuatia kuchapisha picha za Duchess of Cambridge Kate Middleton.

Picha hizo zilichukuliwa wakati wa ziara binafsi ya mapumziko aliyofanya nchini Ufaransa zilichapishwa na Closer mwezi Septemba.


Gazeti moja lilitumia picha zake katika vazi la kuogolea yaani swimwear.

 
Images:  http://www.dailymail.co.uk/
Mondadori boss Ernesto Mauri na wa La Provence Valerie Suau wanafanyiwa uchunguzi wa kuingilia uhuru wa mtu binafsi.

Bi. Suau amekiri kuchukua picha hizo zilizokuwa katika vazi la kuogelea.

MALARIA BADO TISHIO DUNIANI!!

Wakati Jumuiya ya Kimataifa ikiwa inaadhimisha Siku ya Malaria Duniani ifikapo kila mwaka tarehe 25 Aprili, Malaria bado inawakilisha matatizo makubwa ya afya duniani huku nchi 99 zikiendelea kukabiliwa na maambukizi ya ugonjwa huo na watu zaidi ya 650,000 wakifariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa wa Malaria.

Tangu mwaka 2000 kiwango cha vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Malaria kimepungua kwa asilimia 25%. Kuna nchi 50 kati ya nchi 99 zinazoendelea kufanya vyema ili kufikia Malengo ya Maendeleo ya Millenia kwa mwaka 2015 kwa kupunguza vifo kwa asilimia 75%.

Malaria ni ugonjwa unaoendelea kupukutisha maisha ya watu wapatao 660,000 kutoka kila kona ya dunia, wengi wao ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanaoishi Kusini mwa Jangwa na Sahara.

Zaidi ya watu millioni 200 wanashambuliwa na ugonjwa wa Malaria. Kesi nyingi hazipimwi wala kupatiwa tiba muafaka. Dawa zisizo na viwango zinasababisha usugu, jambo ambalo linaweza kukwamisha jitihada za Jumuiya ya Kimataifa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.

Kauli mbiu inayoongoza Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kwa Mwaka 2013; Wekeza kwa siku za baadaye. Shinda Malaria.

Credits: WHO, unmultimedia and AP