Mwili wa marehemu Albert Mangwair, umewasili jijini Dar leo na kuhifadhiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Ngwair ataagwa rasmi na wapenzi na mashabiki wake siku ya kesho Jumatano katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni kuanzia majira ya saa mbili za asubuhi. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kesho hiyo hiyo kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho kutwa Alhamisi.
No comments:
Post a Comment