HOME

Jun 7, 2012

MTOTO ALIYEFUFUKA AKAOMBA MAJI KISHA AKAFA TENA!!

Mtandao mmoja wa habari nchini Brazil umechapisha habari kuwa mvulana mdogo wa miaka miwili ambaye alifariki dunia aliinuka na kukaa ndani ya jeneza kisha akaomba maji na baadae  akalala tena katika jeneza akiwa hana uhai.


Habari hiyo ambayo sio rahisi mtu kuamini, mtandao huo wa ORM umedai kwamba mtoto huyo ambaye ametambulika kwa jina la Kelvin Santos alikuwa hapumui wakati akipatiwa tiba ya homa ya mapafu katika hospitali ya Belem, Kaskazini mwa Brazil Ijumaa iliyopita.


Lakini saa moja kabla ya mazishi ya mtoto huyo siku ya Jumamosi, mtoto huyo marehemu aliinuka na kukaa ndani ya jeneza na kusema kama anaweza kupata maji na familia iliahirisha mazishi kwa saa moja wakiwa na matumaini kuwa angeamka tena, lakini haikutokea na kuamua kumzika
saa kumi na moja jioni siku hiyo.

Jun 6, 2012

BOMU LA KUJITOA MHANGA LAUA 21 AFGHAN!!

Polisi nchini Afghan imeviambia vyombo vya habari kuwa bomu la kujitoa mhanga limeua watu 21 katika shambulio lililofanyika katika hoteli karibu na mji wa Kandahar.


Mkuu wa polisi wa jimbo hilo Abdul Raziq amesema madereva wanaowahudumia majeshi ya NATO walikuwa wanakusanyika katika hoteli hiyo wakati wa shambulio hilo.


Taarifa hiyo ya jeshi la polisi inasema watu 22 walijeruhiwa kufuatia shambulio hilo karibu na uwanja wa ndege wa mji huo.

SARAHA ADONDOKA NA JAMBAZI!!

 
Msanii wa kike aliyeweza kujichanganya vizuri na baadhi ya wasanii wa miondoko ya bongo flava nchini Tanzani, Saraha anayetokea nchini Sweden aendeleza cheche zake kwa kutoa vibao mbalimbali katika gemu hii ya muziki.


Akiwa anatamba na vibao kama Tanesco, Malaika na vinginevyo hivi sasa Saraha amefyatua audio track yake mpya aliyoipa jina 'Jambazi' iliyotayarishwa na mumewe Fundi Samweli katika studio ya Usanii Production.


Isikilize ngoma hapa!!

UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATTA WAFUNGULIWA!!


 Huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya zimerejea katika hali ya kawaida baada ya kusitishwa kwa saa nane kuruka na kutua ndege katika uwanja huo baada ya hitilafu kutokea katika barabara ya kutua na kuruka katika uwanja huo.

Uwanja huo wenye shughuli nyingi ulifungwa saa kumi alfajiri ya leo baada ya ndege ya shirika la ndege la Egypt Air kuvutwa nje ya njia ya kutua ilipokuwa ikitua ikiwa na abiria 123 kutoka Cairo ambao wote walisalimika na kupelekwa katika jengo la uwanja huo.

Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata (KAA) imesema katika taarifa yake kuwa huduma katika uwanja huo zimerejea katika hali yake ya kawaida kuanzia saa sita mchana leo baada ya kutokea hitilafu katika barabara ya kuruka na kutua.