HOME

Feb 3, 2012

MABOMU YA MACHOZI YATAWALA MISRI!!



Waandamanaji waliokasirishwa na vifo vya watu 74 baada ya mchezo wa kandanda katika mji wa Port Said nchini Misri siku ya Jumatano wamepambana na polisi nje ya wizara ya mambo ya ndani mjini Cairo.


Kituo cha TV cha serikali kimesema mamia ya watu wamejeruhiwa katika tukio hilo.


Mapema, waziri mkuu wa Misri alitangaza kuwafukuza kazi maafisa wa ngazi za juu mjini Port Said na pia katika chama cha soka cha Misri.

Mazishi ya baadhi ya waliokufa yamefanyika katika mji wa Port Said.

Feb 1, 2012

POLISI KENYA INAMSAKA MTOTO WA RUPIAH BANDA!!

Henry Banda

Jeshi la polisi nchini Kenya limejiunga katika msako wa mtoto wa rais wa zamani wa Zambia Rupiah Banda ambaye anadaiwa kuwepo nchini Kenya.


Jeshi la polisi nchini Zambia limetoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Henry Banda kufuatia ripoti kuwa amesafiri kutoka Afrika kusini kwenda Kenya baada ya kugundua kuwa anatafutwa kufuatia uchunguzi unaoendelea wa fedha za baba yake za kampeni.


Inspekta generali wa polisi wa Zambia Martin Malama amebainisha kuwa Henry yupo nchini Kenya na kumuonya ajisalimishe kuliko kuendelea kucheza mchezo wa kujificha na sheria.

ICTR YAWAOMBEA HIFADHI WALIOACHIWA HURU!!


Mahakama inayoendesha kesi za mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994 imetoa wito kwa mataifa kutoa hifadhi kwa wale walioondolewa mashtaka.


Watu 5 kati ya watu 10 walioondolewa lawama za kuhusishwa katika mauaji hayo wanasema hawawezi kurejea nchini Rwanda.


Wanaishi chini ya ulinzi wa Polisi katika nyumba moja mjini Arusha, Tanzania, ambako ndiko makao ya mahakama hiyo ya ICTR.


Mahakama hiyo ya ICTR inatarajiwa kufunga mwishoni mwa mwaka huu.

CHADEMA YAITAKA SERIKALI KUREJEA KWENYE MAZUNGUMZO NA MADAKTARI!!

Mkurugenzi wa habari na uenezi chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Bw  John Mnyika

Chama cha  demokrasia na maendeleo Tanzania (CHADEMA)  kimeitaka serikali  kurudi kwenye meza ya mazungumzo  na madaktari na kutumia  rasilimali zilizopo  kutatua madai ya madaktari nchini

Hayo yameelezwa Mkoani morogoro katika kongamano la katiba mpya kwa wananfunzi wa vyuo chuo kikuu Mzumbe ambapo  mkurugenzi wa habari na uenezi chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Bw  John Mnyika amesema kukosekana kwa uadilifu rasilimali zilizopo nchini zinashindwa kuwanufanisha watanzania

Nae Mkurugenzi wa sheria na haki za binadamu  CHADEMA Tundu Lissu akizungumzia kuhusu
katiba mpya amesema watanzania wanahitaji katiba mpya yenye  mabadiliko ya kubadilisha nchi  na kuongeza uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi.