HOME

May 24, 2013

MJUKUU WA MALCOM-X AUAWA, AZIKWA SIKU MBILI BAADA YA BIRTHDAY YA BABU YAKE!

Siku ya tarehe 9 May mwaka huu, dunia ilimpoteza mwanaharakati mwingine Malcom Shabazz ambaye ni mjukuu wa aliyekuwa mwanaharakati wa kimarekani wa haki za binadamu Malcom X.


Malcom Shabazz aliuawa baada ya kutokea ugomvi kwenye bar ya Palace huko Mexico City, kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa na deni la kiasi cha $1,200. Wafanyakazi wawili wa bar hiyo David Hernandez Cruz na Manuel Alejandro Perez de Jesus, wanashikiliwa na polisi kwa mauaji hayo. 

Shabazz alizikwa pembeni mwa babu na bibi yake kwenye makaburi ya Ferncliff Hartsdale New York, tarehe 21 May, ambayo ni siku mbili baada ya birthday ya babu yake Malcom X, ambaye angetimiza miaka 88 kama angekuwa hai leo.

MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI, AMEN!

May 23, 2013

BEN POL AINGIA KIKAANGONI...AKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WAKE KUPITIA FACEBOOK PAGE YA EATV!!

....Akipatiwa maelezo kwa ufupi kutoka Barnaba kutoka kitengo cha New Media EATV

Akichat Livee na Fans wake 
EATV kupitia Facebook Page yake leo imempa nafasi Mwanamuziki mkali wa masauti nchini Tanzania Benpol kuchat Live na mashabiki wake. Hapo amepata nafasi ya kujibu maswali ya kila aina kutoka kwa mashabiki alikuwa kikaangoni.
Ben pia alipata nafasi ya photoshoot na warembo wa EATV 

VIDEO: MWANAUME AMFUMA MKE WAKE AKI - CHEAT...BOYFRIEND ATOROKEA DIRISHANI!!

MZEE WA MIAKA 80 AVUNJA REKODI KUFIKA KILELE CHA MLIMA EVEREST!!

Mzee mwenye umri wa miaka 80 raia wa Japan amefanikiwa kufika kilele cha mlima  Everest kwa mujibu wa timu yake na kumfanya kuwa mwanaume mzee kuliko wote kufika kilele cha mlima huo mrefu kuliko yote duniani.

Kwa mujibu wa timu yake, Yuichiro Miura ambaye alipanda mlima Everest akiwa na umri wa miaka 70 na mara nyingine akiwa na umri wa miaka 75 alifika kilele cha mlima huo mapema siku ya Alhamis asubuhi.

Yuichiro anachukua nafasi ya Bahadur Sherchan ambaye
alifika kilele cha mlima huo akiwa na umri wa miaka 76 mwaka 2008 na kushikilia rekodi hiyo.