HOME

May 3, 2013

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP!!

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa Ushirikiano Wenya Manufaa kwa Wote unaolenga kutafuta mbinu mpya za kukuza uchumi na maendeleo ya kijamii maarufu kama Smart Partnership.







Mkuu wa sekretarieti inayoratibu mkutano huo Bi. Victoria Mwakasege (Katikati) kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa amesema jumla ya wageni 600 kutoka sehemu mbali mbali duniani, kati yao wakiwemo wakuu wa nchi watahudhuria 
mkutano huo utakaoanza Juni 28 na kumalizika Julai Mosi.
Waandishi wa habari wakipata taarifa kuhusu mkutano huo wa Smart Patnership katika Ukumbi wa kurugenzi ya habari na mawasiliano Ikulu, Jijini Dar es salaam.
Meneja wa Sekretariti inayoratibu mkutano huo Bi. Rosemary Jairo akifafanua kwanini Tanzania imeamua kuwa mwenyeji wa mkutano huo na faida itakazopata kutokana na mkutano huo ambapo amewataka waandishi wa habari kuwa wazalendo katika kuripoti habari chanya zinazohusu mambo mbalimbali ya maendeleo.
Bi. Mwakasege amezitaja faida nyingi zitakazopatikana kutokana na mkutano huo kuwa ni pamoja na manufaa ya kiteknolojia hususani namna ya kutekeleza majukumu ya kuihudumia jamii





 

SWAGA ZA SUPAMIX KUELEKEA LOVERS & FRIENDS BATA FRIDAY... NI LEO.... USIKOSE!!!

Hii ni katika kipindi cha Supamix ambapo Baba T (Kulia) DJ mwenye uzoefu wa miaka 46 kwenye game, jana aliamua kutinga studioni kuungana na wana supamix kuwaonjesha burudani itakayoporomoshwa kwenye usiku wa Bata Friday ambao unafanyika leo maisha Club. Tinga kivazi chako cha Red uwakilishe Team Red.

Mtangazaji mahiri Afrika Mashariki Zembwela akitangaza Supamix wakati Baba T anapiga ngoma kalii za Reggae.
Baba T
DJ Kim nae anawakilisha Team Red akiwa na Colletha Raymond wa Show ya weekend breakfast inayoruka kila Jumapili kuanzia saa 12 kamili asubuhi hadi saa nne huwa anakuwa na Michael Lukindo. Kennedy the remedy kwa mbali.
Ireen Tillya aka Bibi ndani ya Supamix na Zembwela.

May 1, 2013

BAADHI YA PICHA ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI JIJINI DAR!!

SHUHUDIA WABUNGE VENEZUELA WALIVYOCHAPANA MAKONDE BUNGENI!!

Wubunnge katika bunge la Venezuela wamepigana ngumi na makonde kufuatia mgogoro wa hivi karibuni wa uchaguzi wa urais nchini humo.

Wabunge kadhaa wameachwa wakiwa na michubuko na damu katika
maeneo kadhaa ya mwili huku wabunge wote wa upinzani na wa chama tawala wakituhumiana kuanzisha ugomvi huo.

Awali maagizo yalitolewa kuzuia wabunge haki ya kuzungumza hadi pale watakapomtambua Nicolas Maduro kama rais wa nchi hiyo.
 Rais Nicholas Maduro.