HOME

May 2, 2012

SERIKALI YAWEKA UDHIBITI KUZUIA WIZI FEDHA ZA UMMA!!

Rais Jakaya Kikwete  amesema wameanzisha utaratibu mpya wa mgao wa fedha za serikali na jinsi zinavyotumika kufuatia hivi karibuni kamati tatu za bunge kubaini matumizi mabaya ya fedha hizo.

Rais Kikwete amesema hayo baada ya kupokea maandamano ya wafanyakazi wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wa mkoa wa Tanga,wafanyakazi wa idara za serikali na viongozi mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi katika kilele cha sherehe za sikukuu ya wafanyakazi duniani Mei mosi zilizofanyika kitaifa mkoani Tanga..

Katika sherehe hizo Rais alitoa vyeti kwa wafanyakazi bora nchini ambapo baadhi yao walielezea kuwa hatua hiyo ni yenye kuwapa ari na tija kwa kulitumikia taifa kabla ya kustaafu cue in nicholaus mganga

KENYA MOURNS WOMEN'S RUGBY CAPTAIN!!

Tributes are being paid to Aberdeen Shikoyi, the captain of the national Kenya Women's Rugby team who died on Saturday in Nairobi.

According to the Kenya Rugby Football Union, Ms Shikoyi was injured during the first leg of the Women's Elgon Cup in Uganda a week earlier.

She was immediately airlifted to the Kenyan capital for treatment, reportedly for a spinal injury.

Her death was announced shortly after her team won this year's Elgon Cup.

WABUNGE WAWILI SOMALIA WAFA KWENYE MLIPUKO!!

Mamlaka katika mji wa Dusa Mareb nchini Somalia zimesema takribani watu saba wakiwemo wabunge wawili wameuwawa katika shambulio la bomu katikati ya nchi hiyo.

Mashuhuda wa  tukio hilo wameliambia shirika la habari la BBC kuwa shambulio hilo lilikuwa limelenga kikundi cha wanasiasa 20 waliokuwa katika mgahawa wa wazi.

Wanasiasa hao walikuwa wamesafiri kwenda mji wa Dusa Mareb uliopo Galgadud unaodhibitiwa na majeshi yanayounga mkono serikali ya nchi hiyo kuhamasisha mapatano.

Kikundi cha kiislamu cha Al-Shabaab kimesema kimehusika na shambulio hilo.

WAVULANA WATAMBA MATOKEO KIDATO CHA SITA!!

Dk Joyce Ndalichako
Baraza la Mtihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita iliyofanyika Februari mwaka huu yakionyesha kuongezeka kidogo kwa kiwango cha ufaulu kwa ujumla huku wavulana waliofaulu wakiwaacha mbali wasichana.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Joyce Ndalichako, kati ya watahiniwa 46,499 waliofanya mtihani huo,  wavulana waliofaulu ni 30,466 wakati wasichana ni 16,033. Hata hivyo, kumekuwa na mchuano mkali katika ufaulu kwa asilimia ambao wasichana walipata 87.37 na wavulana 87.69.

Sekondari ya Wasichana ya Marian, Bagamoyo ndiyo iliyoongoza kitaifa na mwanafunzi wake, Faith Assenga ndiye aliyeshika namba moja katika masomo ya Sayansi.

“Katika masomo ya Biashara, aliyeshika nafasi ya kwanza ni Alex Isdor wa Sekondari ya Kibaha na Lugha ni Faridi Abdallah wa Sekondari ya Mpwapwa,” alisema Dk Ndalichako.

Dk Ndalichako alisema kiwango cha kufaulu kwa watahiniwa 46,499; wakiwemo wale wa kujitegemea, kimeongezeka kutoka asilimia 87.24 mwaka jana hadi 87.58 mwaka huu.