HOME

Apr 30, 2013

BIDHAA ZA VYAKULA TANZANIA ZIMEKUWA KIVUTIO KIMATAIFA!!

Tanzania imetakiwa kuwa makini na kuchukua hatua dhidi ya baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchi za jirani, ambao huingia nchini na kununua mazao kwa njia za magendo na baadaye kwenda kuuza nchi za nje huku wakijinadi kuwa kuwa mazao na bidhaa hizo zimetoka katika nchi zao.
Viongozi wa Trade Africa Network Tanzania wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es saalam. Kushoto ni Councelor wa Mtandao huo Bi. Muna Masesa na Mwakilishi mkazi wa mtandao unaojishughulisha na ukuzaji uchumi na mauzo ya bidhaa nje ya nchi wa Trade Africa Network Tanzania Bw. Deusdedit Kizito
Mwakilishi mkazi wa mtandao unaojishughulisha na ukuzaji uchumi na mauzo ya bidhaa nje ya nchi wa Trade Africa Network Tanzania Bw. Deusdedit Kizito, akizungumza leo jijini Dar es Salaam
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakitekeleza majukumu yao.

Mwakilishi mkazi wa mtandao huo Bw. Deusdedit Kizito, amesema kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikiinyima Tanzania fursa ya kunufaika na masoko ya kimataifa.

Katika kukabiliana na hali hiyo, Deusdedit ameishauri serikali kuhakikisha inatunga sera na sheria ya matumizi bora ya ardhi, ambayo pamoja na mambo mengine, itasaidia kuepusha utoroshwaji wa mazao lakini pia itatenganisha kati ya kilimo hai na kile cha kisasa.

MSONGAMANO MKUBWA WA MAGARI BARABARA YA KIJITONYAMA!!


Kutokana na mvua za hapa na pale zilizonyesha leo katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam, Hali imeonekana kuwa mbaya kwa upande wa barabara ambapo kumeonekana msongano katika baadhi ya maeneo uliosababisha kero kubwa kwa watumiaji wa barabara kutokana na foleni kubwa. 
Hii ni barabara ya Mwananyamala Kijitonyama inavyoonekana leo katika picha ambapo magari kadhaa yalionekana kukwepa foleni iliyokuwa katika barabara kuu ya Alli Hassan Mwinyi na Mwai Kibaki.

ELSIE KANZA MTANZANIA PEKEE KWENYE ORODHA YA WANAWAKE MAARUFU 60 AFRICA!!

 
Mtandao wa Women, Inspiration and Enterprise (WIE) umezindua orodha yake ya wanawake wenye ushawishi mkubwa Afrika kuelekea kongamano lake litakalofanyika Cape Town Mei mwaka huu.

Rais wa Malawi Bi.  Joyce Banda, Mke wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Bi. Graça Machel  
Mwanamitindo wa kimataifa na mjasiriamali Iman, Mwanaharakati Dr Mamphela Ramphele, Mwandishi wa kimataifa  Chimamanda Ngozi Adichie na mwigizaji Thandie Newton wote wameingia katika orodha hiyo ya wanawake 60 maarufu barani Afrika.

Mkutano wa WIE ulitoa orodha hiyo iliyowataja wanawake wenye ushawishi mkubwa barani Afrika ambapo mtandao huo huwatambua wanawake ambao mafanikio yao yamekuwa chachu ya mabadiliko Afrika na duniani kwa ujumla.

Elsie Kanza
Katika orodha hiyo, Mtanzania Elsie Kanza ambaye ni Head of Africa, WEF amefanikiwa kuingia. Bi. Kanza ameingia kupitia kipengele cha PHILANTHROPY AND ADVOCACY akiwa pamoja na
Graca Machel - Humanitarian, Mozambique
    Ellen Johnson Sirleaf - President of Liberia
    Elsie Kanza - Head of Africa, WEF. Tanzania
    Fatou Bensouda - Chief prosecutor, Intl Criminal Court. Gambia
    Hadeel Ibrahim - Philanthropist
    Jeanette Kagame - 1st Lady of Rwanda
    Joy Phumaphi - VP, Human Development Network, World Bank
    Joyce Banda - President of Malawi
    Leymah Gbowee - Activist, Liberia
    Dr Mamphela Ramphele - Activist, Academic, Businesswoman
    Toyin Saraki - Founder, Wellbeing Foundation Africa. Nigeria
    Nkosazana Dlamini Zuma - Chair, African Union Commission

Julie Gichuru
Pia katika orodha hiyo Mwanamke maarufu Julie Gichuru amefanikiwa kuingia kupitia kipengele MEDIA AND CULTURE ambacho kinatuhusu wanahabari wanawake kwa kiasi kikubwa akiwa pamoja na wanawake maarufu kutoka nyanja mbalimbali akiwemo Dambisa Moyo - Writer, economist, Angelique Kidjo - Musician, Activist. Benin, Biola Alabi - Managing Director, MNET Africa, Chimamanda NgoziAdichie - Author
    Isha Sesay - Anchor, CNN
    Julie Gichuru - Journalist. Kenya
    Khanyi Dhlomo - Founder, Destiny Magazine
    Mariam Doumbia - Musician
    Oumou Sangaré - Musician. Mali
    Patricia Amira - Talk Show Host. Kenya
    Yvonne Chaka Chaka - Musician. South Africa
    Tsitsi Dangarembga - Novelist, screenwriter. Zimbabwe.

Kwa mengine zaidi unaweza kutembelea: https://www.wienetwork.org/africa-power-list-2013/

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA KUTOA RASIMU YENYE MASLAHI KWA TAIFA!!

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo  Kulia ni Katibu wa Tume, Bw. Assaa Rashid. (Picha na Tume ya Katiba)
Na Mwandishi Tume ya Katiba.

Tume ya Mabadiliko ya Katiba imesema imejipanga kuandaa rasimu ya katiba itakayoweka mbele maslahi ya taifa na kuwaomba wananchi waijadili na kutoa maoni yao katika mabaraza ya katiba yatakayokutana kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jospeh Warioba amesema leo jijini Dar es Salaam  kuwa katika kuandaa rasimu hiyo, Tume yake haitapokea shinikizo kutoka taasisi, asasi, makundi au vyama vya siasa.

“Tume haitengenezi katiba ya vikundi au vyama, tunaandaa katiba ya nchi,” amesema Jaji Warioba katika mkutano wake na waandishi wa habari katika ofisi za Tume na kufafanua kuwa Tume inazingatia uzito wa hoja zilizotolewa  na wananchi na sio idadi ya watu waliotoa maoni.

Jaji Warioba amewataka wananchi kutokubali kutumiwa na makundi, asasi, taasisi na vyama wakati wa kujadili na kutoa maoni katika mabaraza ya katiba ya wilaya.
Mwenyekiti wa kamati ya uwasilishaji wa mapendekezo ya muundo wa mabaraza ya Katiba kwa jamii ya watu wenye ulemavu, Bw. David Nyendo (kushoto) akiwasilisha maoni yake ya kamati hiyo kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao uliofanyika  ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa Tume, Dkt. Salim Ahmed Salim. (Picha na Tume ya Katiba)
Akizungumza kuhusu ushiriki wa walemavu katika mabaraza ya katiba, Jaji Warioba amesema Tume yake inatarajia kuunda mabaraza ya Katiba ya watu wenye ulemavu ili kuwapa fursa walemavu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kutoa maoni yao kuhusu rasimu ya Katiba itakayotolewa na Tume.

Hatua hii inafuatia ombi la Shirikisho la Vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) na Umoja wa Watu wenye ulemavu Zanzibar (UWAZA) waliloliwasilisha kwa Tume.

Aidha, Jaji Warioba amezungumzia mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika chaguzi zilizofanyika nchini kote hivi karibuni za kuchagua Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba kuanzia ngazi ya mitaa, vijiji, vitongoji na shehia.

Kwa mujibu wa Jaji Warioba, tathmini ya Tume inaonyesha kuwa kwa kiwango kikubwa viongozi na watendaji katika ngazi za vijiji, mitaa, shehia na kata walizingatia mwongozo uliotolewa na Tume na kuwa maeneo mengi wananchi walichaguana kwa amani na utulivu.

“Kwa mfano jumla ya shehia 323 sawa na asilimia 96.4 kati ya shehia 335 kwa upande wa Zanzibar zimekamilisha vizuri mchakato huu, hali kadhalika jumla ya Kata 3,331 sawa na asilimia 99.8 kati ya Kata 3,339 kwa Tanzania Bara nazo zimekamilisha mchakato wa kuwapata wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kwa kuzingatia utaratibu uliotolewa kwa mujibu wa Mwongozo,” amesema Jaji Warioba.

TAZAMA MAKALA YA KUSISIMUA ''UOZO KATIKA JAMII'' BINTI ANAYEJIUZA HUKU AKIWA ANASOMA!!

Apr 29, 2013

LHRC KUTOA RIPOTI YAKE YA HAKI ZA BINADAMU!!

Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania kwa kushirikiana na kituo cha huduma za kisheria visiwani Zanzibar, kwa pamoja kesho watatoa ripoti ya hali ya haki za binadamu nchini.

Taarifa ya kituo hicho imesema kuwa ripoti hiyo ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita, itaangalia namna sera na sheria zilizopo zilivyoshindwa kukabiliana na ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu.

Aidha ripoti hiyo imefafanua kuwa ripoti hiyo itatoa ushauri wa hatua zinazopaswa kuchukuliwa na jamii pamoja na serikali, katika kukabiliana na matukio ya uvunjaji wa haki za binadamu ambayo yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka.

NAMELESS SUPPORTS #TEAM RED @LOVERS & FRIENDS BATA FRIDAY !!

 
Star wa Muziki Afrika Mashariki kutoka nchini Kenya Nameless ameamua kuvunja ukimya na kuweka wazi kuwa yeye binafsi kutoka moyoni anaipa Support Team Red ambayo inawakilisha show kalii kutoka East Afrika Radio yaani Suparmix, EA Breakfast pamoja na ma Dj wa Team hiyo Baba T na Big Man Kim.

Bado hujachelewa una nafasi kubwa ya kushow love kwa kusupport Team hii ambayo imeonekana kukonga nyoyo za watu na kujizolea mashabiki lukuki tangu kutangazwa kwa kampeni ambazo kilele chake ni siku ya Ijumaa pale Maisha Club kwa kiingilio cha elfu 10 tu mlangoni na uje na Dress Code ya kuwakilisha Team yako.

Guest DJ ni Baba T ambaye ana uzoefu wa takribani miaka 46 kwenye game! Ataporomosha ngoma kali za reggae usije ukachelewa. Binafsi na Support Team Red kama Nameless wewe unawakilisha rangi gani?????

WATUMISHI WAZEMBE WALA RUSHWA KUADHIBIWA!!

Watumishi wa umma nchini Tanzania wametakiwa kuacha vitendo vya rushwa na kufanya kazi kwa mazoea ili kuiwezesha nchi kufikia malengo ya maendeleo ya muda mrefu.
Waziri wa nchi ofisi ya rais Utumishi Celina Kombani akifungua mafunzo kwa maofisa waandamizi wa umma kuhusu namna wanavyoweza kutekeleza majukumu yao leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa nchi ofisi ya rais Utumishi Celina Kombani akifungua mafunzo kwa maofisa waandamizi wa umma kuhusu namna wanavyoweza kutekeleza majukumu yao.
Baadhi ya maofisa waandamizi wa umma waliokuwa katika mafunzo hayo kuhusu namna wanavyoweza kutekeleza majukumu yao.
Waziri wa nchi ofisi ya rais Utumishi Celina Kombani akiwa katika mafunzo hayo aliyofungua leo Jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Waziri wa nchi ofisi ya rais utumishi wa umma, Celina Kombani, akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa maofisa waandamizi wa umma, kuhusu namna wanavyoweza kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia malengo hayo.
Katika maelezo yake, waziri Kombani amewataka watumishi wa umma kuacha vitendo vya rushwa kwani serikali haitosita kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria kwani vitendo hivyo vimekuwa vikikwamisha juhudi za serikali za kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

SAD NEWS...KIFO CHA MWANASHERIA MUTULA KILONZO KENYA!!

Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla imekumbwa na huzuni kubwa kufuatia taarifa za kifo cha aliyekuwa Seneta wa Jimbo la Makueni na mwanasheria maarufu Mutula Kilonzo aliyekutwa amekufa nyumbani kwake mapema siku ya Jumamosi.

Uchunguzi wa mwili wake unatarajiwa kufanyika leo pale Lee Funeral Home ambapo,
Mwili wa mwanasiasa huyo ulipelekwa katika nyumba hiyo kwa ajili ya kuhifadhiwa Jumamosi usiku baada ya kukutwa amefariki nyumbani kwake katika ranchi ya Maanzoni iliyopo kaunti ya Machakos.

Mwanasayansi mkuu wa elimu ya magonjwa (Mwanapatholojia), Dk.  Johansen Oduor atafanya uchunguzi huo akishuhudiwa na wanafamilia wa marehemu Kilonzo na aliyekuwa daktari wake.

Matokeo ya uchunguzi huo yanatarajia kutolewa kesho ambapo taarifa za awali zinaonyesha kuwa hakukuwa na majeraha yoyote katika mwili wake.

Vyanzo vya habari vimesema kuwa kuna uwezakano Marehemu Kilonzo akazikwa siku ya Ijumaa wiki hii wakati uchunguzi wa kifo chake ukiendelea.

Pichani: Aliyekuwa makamu wa rais Kenya Kalonzo Musyoka akimpa pole Kethi Kilonzo mtoto wa aliyekuwa Seneta wa Jimbo la Makueni Mutula Kilonzo. Picha na StandardMedia

 Kilonzo ni baba wa mwanasheria maarufu Kenya, Kethi Kilonzo ambaye katika siku za hivi karibuni aligusa mioyo ya wakenya wengi katika mitandao ya kijamii na kuwa kivutio cha wengi wakati wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais.

 Kethi alikuwa na akiwakilisha upande taasisi isiyo ya kiserikali ya Africog na kufananishwa sana na baba yake kutokana na umahiri wake aliounyesha katika kesi hiyo.

Hii hapa ni taarifa ya Televisheni cha Citizen Kenya ikielezea zaidi kuhusiana na kifo cha Mheshimiwa Mutula Kilonzo.

SARAFU MOJA CHANGAMOTO EAC!!

Viongozi wa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamemaliza mkutano wao mkuu wa 11 nje kidogo ya  jiji la Arusha nchini Tanzania bila ya kufikia uamuzi juu ya kutekelezwa kwa makubaliano ya soko la pamoja na kuanzishwa kwa sarafu ya pamoja katika nchi za Jumuiya hiyo.

Viongozi hao wamerudisha ripoti na kuwataka mawaziri wao kutatua masuala kadhaa yaliyobaki ambapo Hata hivyo viongozi hao kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda Burundi na Rwanda wamesisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha mazingira ya biashara huru na uwekezaji katika Jjumuia yao.

Katika mkutano huo, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alipata nafasi ya kutoa hotuba yake ya kwanza tangu achaguliwe kuwa rais mpya wa Kenya ambapo kati ya  mengi aliyozungumza ametoa wito wa kuharakisha kutataua vikwazo vinavyodhoofisha mchakato mzima wa kuunda Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Apr 27, 2013

TOKELEZEA NA TEAM RED @LOVERS & FRIENDS BATA FRIDAY!!

 
Red is the warmest of all colors. Red is the color most chosen by extroverts and one of the top picks of males. Red is the color of prosperity and joy.

It brings focus to the essence of life and living with emphasis on survival. Red is also the color of passion, Courage and respect, Job well done, Congratulations.

Put some red in your life to increased enthusiasm and interest, more energy, action and confidence to go after your dreams, protection from fears and anxietie.

Join Team Red Uwakilishe:

 
EA Breakfast Show inayoruka kila siku za Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tatu.

Supamix '' Sahani ya Jamii'' inayoruka kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa saa tatu kamili asubuhi hadi saba mchana.

Tokelezea na outfit kalii ya Red kuwakilisha Team yako na pale utakutana na wajanja wenzako kibaooo wakiwa wametupia vitu vya Red kuwakilisha EA breakfast na Supamix bila kusahau Dj mkali Afrika Mashariki Baba T na DJ Big Man Kim.

WALE WA KULA BATA....LOVERS & FRIENDS BATA FRIDAY!!! HII HAPA UTAWAKILISHA RANGI GANI????


East Africa Radio inakuletea Lovers & Friends Bata Friday"itakayofanyika pale Club Maisha siku ya Ijumaa ya kwanza ya mwezi May tarehe 3, 2013.  

Dress code ni Red, White and Yellow. Team tatu kali zimeundwa ambapo Red itawakilisha Show kali za EA Breakfast na Supermix ikipewa suport na ma DJ wakali DJ Kim na Baba T ambaye ataporomosha ngoma kali za reggae (Ragga Muffin, Sweet raggae etc). 

Team White itawakilisha Power Jams na EA Drive itakayopewa support na Dj Summer na Dj 45 King na Team ya tatu Team Yellow itawakilisha The Cruise na Late Night na kupewa support na Dj Mafuvu pamoja na Dj Mackay. 

Njoo ukiwa umevalia rangi itakayowakilisha kipindi chako ukipendacho kutoka East Africa Radio

Elfu 10 yako tu pale mlangoni @Club Maisha.
Utawakilisha rangi gani????
 
East Africa Radio '' Together Tunawakilisha''

EXCLUSIVE PHOTOS: MARKETER'S NIGHT OUT @GOLDEN TULIP HOTEL!!

 Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker Lite iliandaa hafla maalum ya maafisa masoko '' Marketer's Night Out iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip siku ya Alhamis na kuhudhuriwa na maafisa masoko kutoka makampuni mbalimbali ambapo msemaji mkuu alikuwa Dk. Wale Akinyemi kutoka Nigeria ambaye alitoa mafunzo muhimu sana kwa ustawi wa makampuni mengi hapa nchini.
Hawa ni warembo ambao walihusika katika kukaribisha wageni waliofika katika hafla hiyo iliyofana sana pale Golden Tulip.

Maafisa masoko kutoka makampuni mbalimbali wakiwa wamejumuika katika picha ya pamoja na Msemaji mkuu katika hafla hiyo ya Marketer's night out Dk. Wale Akinyemi kutoka Nigeria.
Msemaji mkuu (Key speaker) katika hafla hiyo ya Marketer's night out Dk. Wale Akinyemi kutoka Nigeria akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya bia Serengeti kupitia kinywaji cha Tusker Lite.

Msemaji mkuu katika hafla hiyo ya Marketer's night out Dk. Wale Akinyemi kutoka Nigeria akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya bia Serengeti kupitia kinywaji cha Tusker Lite.


Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti Steve Gannon akiwakaribisha wageni waalikwa katika hafla hiyo kubwa na nzuri ambayo hufanyika mara kwa mara ya Marketer's night Out.

Mkurugenzi wa masoko wa SBL Mr. Ephrahim Mafuru akizungumza machache katika hafla hiyo


Mtangazaji maarufu kutoka East Africa Radio ambao walikuwa wadhamini wakuu kwa Upande wa Media, Hillary Daudi ''Zembwela au Babu'' kutoka kipindi cha Supamix akinadi kipindi chake mbele ya maafisa masoko waliohudhuria hafla hiyo ya Marketer's night out.

Katika hafla hiyo kulikuwa na vyakula vya kila aina kukamilisha shughuli nzima ambapo watu walisevia vya kutosha tu.



Watu walipata misosi ya nguvu na kushushia na kinywaji rasmi cha usiku huo Tusker Lite


Pichani kulia: Hillary Daudi maarufu kama Zembwela akiwa na Patner wake katika kazi Ireen Tillya ''Bibi'' ambao wote ni watangazaji wa kipindi maarufu cha Supamix kinachorushwa kila siku za wiki Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa saba kamili mchana.


Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.

Wafanyakazi wa EATV kutoka upande wa Marketing wakiwa katika hafla ya Marketer's night out iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip.


Wageni kutoka makampuni mbalimbali kulia ni mtangazaji wa kipindi cha Nirvana Deogratius Joseph Kithama na Ziada Abeid kutoka Push Mobile pamoja na rafiki.





B Band wakiongozwa na Banana Zorro ndio walikuwa watumbuizaji wakuu katika haflya hiyo ambapo waliporomosha burudani nzuri unaweza kujionea mwenyewe katika picha jinsi Dancing Floor ilivyosheheni.