Feb 6, 2012
JIJI LA NAIROBI KUENDELEA KUWASAKA MAKAHABA!!
Meya wa jiji la Nairobi George Aladwa ametangaza jana kuwa baraza lake litaendelea kuwasaka makahaba wakati baraza hilo likiendelea kusubiri mapendekezo ya kamati iliyoundwa kujadili ikiwa ukahaba unaweza kuhalalishwa.
Meya Aladwa amesema suala la biashara ya ukahaba ni haramu kulingana na sheria za nchi na kuainisha kwamba wataendelea kuwakamata makahaba pamoja na wateja wao mpaka hapo mapendekezo ya kamati itakapoainisha juu ya suala hilo.
Wiki iliyopita meya huyo alitangaza hatua ambazo zimechukuliwa na baraza za kutenga maeneo ambayo yatatumika kwa ajili ya bishara ya ukahaba kwa sababu makahaba wamekuwa wakilalamika kubughudhiwa na askari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment