HOME

Apr 24, 2012

SYRIAN INTELLIGENCE OFFICER KILLED IN DAMASCUS ATTACK!!

Photo released by Syrian news agency SANA shows blood on pavement next to damaged truck after car bomb in Damascus. 
Activists say a Syrian intelligence officer has been shot and killed in the capital, Damascus, while a separate bomb blast wounded three people in the city.


The attacks come amid fears that Syria's 13-month conflict is growing increasingly militarized, and diplomatic efforts to solidify a tenuous cease-fire continue.


The Britain-based Syrian Observatory for Human Rights said the officer was killed early Tuesday in the Barzeh neighborhood but gave no further information. The Syrian government did not comment.

AY KUSHUSHA MZIGO WA BEI MBAYA!!

AY
Nyota wa muziki Tanzania Ambwene Yesaya AY, amethibitisha kuwa atafanya video ya kiwango cha hali ya juu huko Afrika Kusini kati ya mwezi ujao kwa kollabo yake kali ambayo ameifanya na mtayarishaji muziki Marco Chali kutoka hapa hapa Tanzania.


AY amesema kuwa video hii itaongozwa,upigajipicha na marekebisho hadi kukamilika na kampuni maarufu ya Godfather ambayo pia ndio imehusika vilivyo katika kutengeneza video kali za wasanii wakali kama vile P Square na Mr Flavour kutoka Nigeria.

MVUA ZIMESABABISHA MAAFA NCHINI KENYA!!

Mvua zilizoanza kunyesha nchini Kenya zimeendelea kusababisha maafa ya vifo na uharibifu wa mali kwa wananchi huku kitengo cha mamlaka ya hali ya hewa nchini humo kikionya uwezekano wa kutokea mafuriko zaidi.

Wananchi wa Kenya wameshauriwa kutoa tahadhari kwa mamlaka husika wakati kukiwa na tishio la mafuriko katika maeneo ya jirani wakati mvua kubwa zikiwa zinaendelea kunyesha nchini humo.

Siku ya Jumatatu miili ya watu sita ilipatikana kutoka hifadhi ya taifa ya Hell's Gate huko Naivasha ambako waumini saba vijana waliokuwa wakifanya ziara kusombwa na maji siku ya Jumapili.

Maeneo yaliyotambuliwa na mamlaka ya hali ya hewa kukumbwa na mafuriko ni pamoja na Budalangi,Nyando, Elgeyo Marakwet, Baringo, Nairobi na mikoa ya Murang’a.

Apr 21, 2012

RAIS WA MAREKANI ATAKA MAPATANO SUDAN!!

Majeshi Sudan Kusini.






















Rais Obama ametoa wito kuwa mapigano baina ya Sudan Kaskazini na Kusini yamalizwe, na marais wa nchi zote mbili wawe na ujasiri wa kutatua tofauti zao kwa amani.


Rais Obama amesema Sudan Kaskazini inafaa kusitisha hatua za kijeshi dhidi ya jirani yake pamoja na mashambulio ya ndege; na Sudan Kusini iache kusaidia makundi yenye silaha ndani ya Sudan Kaskazini, na harakati zake za kijeshi mpakani.


Baada ya Sudan Kusini kuviteka visima vya mafuta kwenye eneo la Heglig la mpakani siku kumi zilizopita, nchi hizo zilikaribia vita, lakini majeshi yake yameondoka, baada ya malalamiko ya kimataifa.