Mar 23, 2012
CAUSES OF WHITNEY HUOSTON DEATH REVEALED!!
Whitney Houston’s death was caused by accidental drowning, but drug abuse and heart disease were also factors.
Coroner’s spokesman Craig Harvey said drug tests indicated the 48-year-old US singer was a chronic cocaine user.
The announcement ends weeks of speculation over the cause of Houston’s death.
She was found submerged in the bath of her Los Angeles hotel room on the eve of the Grammy Awards on 11 February.
In a statement, the LA County Coroner’s office described Houston’s manner of death as an “accident”, adding that “no trauma or foul play is suspected”.
The cause was cited as drowning and “effects of atherosclerotic heart disease and cocaine use”.
Other drugs found in her blood included marijuana, as well as an anti-anxiety drug, a muscle relaxant and an allergy medication.
AFANDE SELE AWACHANA VINEGA...AIFANANISHA BONGO FLEVA NA SHAMBA AMBALO SASA LIMEISHA RUTUBA!!
![]() |
| Mkali wa Rymes Afande Sele akiwa na Fadhili Kiwia kutoka dawati la Enews ya EATV na Michael Lukindo kutoka The Requeast Show ya East Africa Radio. |
![]() |
| Afande Sele pamoja na Zembwela kutoka Super mix ya East Africa Radio. |
![]() |
| Afande Sele akiwa na Michael Baruti (kushoto) na Zembwela (Kulia) |
![]() |
| Afande Sele pamoja na Music Coordinator wa East Africa Radio Big Man Kim ''DJ KIM'' |
Mkali wa Rymes msanii wa Bongo Fleva Dume la Simba Afande Sele amefunguka mengi kuhusu muziki kwa ujumla baada ya kimya cha muda mrefu wakati akizungumza na blog hii leo pamoja na shutuma mbalimbali alizopata kuwa yeye ni msaliti wa kundi la Vinega na kudai kuwa yeye na Mh. Joseph Mbilinyi ''Sugu'' ndio waanzalishi wa kundi hilo lakini ''Mchwa'' ants wa kundi hilo ndio wanafiki kwa kuwa wamefanya mengi ikiwemo kumnyima shoo zilizokuwa zikiandaliwa na kundi hilo katika mikoa mbalimbali kama Mbeya na lile la Uzinduzi wa Albam ya Anti Virus lililofanyika katika viwanja vya Ustawi wa jamii hivi Karibuni.
Amemshushia shutuma Soggy Doggy na kusema anamshangaa jinsi alivyo ni mtu wa ajabu na anahitaji kuombewa kwani ni mnafiki na yeye ndio chanzo cha yote haeleweki''.
Afande amesema yeye ni mfalme na kamwe hawezi kuishiwa pamoja na maneno ya shutuma nyingi juu yake za kufeli na kupotea katika Game na hata kuwa anambania Dogo Ditto wakati ni mdogo wake na sasa anafurahia mafanikio na matunda ya Ditto.
Afande Sele pia amefunguka kushusu muziki wa Bongo Fleva ambapo amesema na kusema muziki huo ambao ni shamba sasa limeisha rutuba kwani yamebaki makapi mwanamuziki wa mwisho kuzalishwa kwenye shamba hilo ni Fid Q wanaofuata hawajui nini wanafanya na kuwaita ''Maua Saa sita''
Sele amesema ''Mwanamuziki ni sawa na ua ndani ya bustani kubwa ya Muziki, kazi kwako kuchagua unataka uwe ua la aina gani!! MauaSaaSita Mjipange''
Mar 22, 2012
''WAZEE WA NGWASUMA'' BENDI YA FM ACADEMIA KUNOGESHA BONANZA LA WANAHABARI JUMAMOSI!!
Bendi ya muziki wa Dansi nchini FM Academia "Wazee wa ngwasuma" wanatarajiwa kutoa burudani ya kukata na shoka katika Bonanza la waandishi wa habari linalotarajiwa kufanyika Jumamosi hii ambapo wanahabari zaidi ya 1500 kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari nchini wanatarajiwa kushiriki katika Bonanza hilo litakalofanyika katika ukumbi wa msasani Beach Club.
Bonanza hilo hufanyika kila mwaka likiandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na linajulikana kama Media Day Bonanza.
Lengo la bonanza ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari, ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja.
Maandalizi kuhusiana na bonanza hilo yapo hatua za mwisho, ambapo shughuli itaanza saa tatu asubuhi hadi saa mbili usiku.
Pamoja na FM Academia pia kutakuwa na wanamuziki wa Bongo Fleva ili kuongeza nguvu ya burudani.
Mgeni rasmi katika bonanza hili atakuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki na aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta.Pamoja na mambo mengine, Sitta atakabidhi zawadi za vikombe na medali kwa washindi mbalimbali watakaoibuka siku hiyo, pia atapata fursa ya kuzungumza na washiriki wa bonanza hilo.
RAIS KIKWETE AONGOZA KILELE CHA WIKI YA MAJI IRINGA LEO!!
![]() |
| Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mitambo na eneo la kusafisha maji yanayotumika katika mji wa Iringa na vitongoji vyake huko Ndauka, katika manispaa ya Iringa mjini leo asubuhi. |
Subscribe to:
Posts (Atom)








