

Kati ya madhara yaliyotokea kufuatia vurugu hizo ni pamoja na kuchoma Ofisi ya mbunge wa chama cha mapinduzi ambayo imeharibiwa vibaya, mahakama ya mwanzo imechomwa na kuteketea kabisa, Nyumba ya askari polisi imechomwa, nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC ilichomwa ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Karim Shaibu amefariki dunia na askari wawili kujeruhiwa.
''Mpaka sasa Watuhumiwa 91 wamekatwa kwa kuhusika na mikusanyiko isiyo na kibali ambapo Wakati huo askari wanne walipoteza maisha wengine kujeruhiwa wakati wakiwa njiani kwenda kulinda maisha ya watanzania mkoani Mtwara na kwakuwa waliumia wakiwa kazini damu yao haitamwagika bure''. Nchimbi
Nchimbi amesema suala hilo limekwishazungumziwa sana ikiwemo faida zake na usafirishwaji wake kwa uchumi wa nchi. Wasaliti wanatumia vibaya uelewa wetu mdogo kuhusiana na gesi hivyo tusikubali kuyumbushwa.
Kufuatia suala hilo, Spika wa bunge la Tanzania Mhe. Anna Makinda amelazimika kuahirisha shughuli za bunge hadi kesho saa tatu asubuhi na kuitaka kamati ya uongozi kukutana kujadili kwa kirefu zaidi suala hilo kuhusiana na vurugu zilizotokea jana mkoani Mtwara.
Picha kwa hisani ya
No comments:
Post a Comment