
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohamedi Gharib Bilal amezitaka nchi za Afrika kuungana kwa pamoja, kutafuta suluhisho la tatizo la uhalifu wa mitandao ambalo limeonekana kukua kwa kasi katika nchi hizo.
Makamu wa Rais amesema hayo leo jijini Dar-Es-Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa sekta ya mawasiliano kutoka nchi mbali mbali za Afrika ukiwa na lengo la kujadili jinsi sekta hiyo inavyoweza kusaidia katika maendeleo ya nchi zao.
Makamu wa Rais amesema tatizo hilo haliwezi kutatuliwa na nchi moja, kutokana na sekta ya mawasiliano kukua, hivyo ni vema nchi hizo zikaungana na kutafuta ufumbuzi wa namna ya kulidhibiti.

No comments:
Post a Comment