Spika wa bunge la Tanzania Mhe. Anna Makinda amesitisha kikao cha bunge tofauti na ilivyotarajiwa na kuiruhusu kamati ya kanuni za bunge kwenda kuijadili hotuba ya bajeti ya kambi ya upinzani kuhusu wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo.
Hatua Hii imekuja baada ya hotuba hiyo kuanza kwa maneno yaliyodaiwa kuwa ya kichochezi yaliyomo ndani ya hotuba hiyo ambapo Mhe. Joseph Mbilinyi alikuwa akiwasilisha hotuba yake.
Hii si mara ya kwanza kwa spika Makinda kutoa uamuzi wa kuitaka kamati ya kanuni kuifanyia mapitio hotuba ya kambi ya upinzani kuona kama inaweza kufanyiwa marekebisho kabla ya kusomwa bungeni.
Hii si mara ya kwanza kwa spika Makinda kutoa uamuzi wa kuitaka kamati ya kanuni kuifanyia mapitio hotuba ya kambi ya upinzani kuona kama inaweza kufanyiwa marekebisho kabla ya kusomwa bungeni.
No comments:
Post a Comment