HOME

Jun 5, 2013

PICHA: MAPOKEZI YA MWILI WA MAREHEMU NGWAIR LEO JIJINI DAR-ES-SALAAM







Mwili wa marehemu Albert Mangwair, umewasili jijini Dar leo na kuhifadhiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. 

Ngwair ataagwa rasmi na wapenzi na mashabiki wake siku ya kesho Jumatano katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni kuanzia majira ya saa mbili za asubuhi. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kesho hiyo hiyo kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho kutwa Alhamisi.

Jun 3, 2013

BRAND NEW ONLINE SHOW: VIDEO SURGERY!! (WATCH)

VIDEO SURGERY, Show mpya ambayo itaanza kuwa published Youtube, Mpango na lengo lake kubwa likiwa ni kujenga na kuboresha kazi mbalimbali za videos zinazofanya na wasanii, hususan Music Videos, Kwa kushirikisha wataalam wa Video Production kwa karibu pamoja na maoni ya kwako wewe mkali wetu, tutakuwa tunachambua videos ambazo kwa mwanzo huu tutakuwa tunazichagua sisi na kuhighlight mambo yoote ambayo yamefanyika vizuri katika video hiyo na pia tutakuchana kinomanoma pale ambapo tutakuwa tumeona makosa dhahiri, lengo kubwa likiwa ni kuwachallenge wasanii kufanya kazi bora zaidi kwa mashabiki wao.

Presenters wa show ni Kennedy Frank Remedy [@KenedyFrank] na Fadhili Kiwia [Mo_Faze] chini ya Director mkali Edson Kato 2.5D [.....], Mpango ndio umekaa hivi na maoni na support yako ni muhimu sana katika kufanikisha hili.

Find and Like us on Facebook kupitia link hii https://www.facebook.com/VideoSurgery na pia twitter kupitia https://twitter.com/CreativemindsTZ na pia blogspot http://videosurgerytz.blogspot.com/.

Kwa followup Subscribe youtube channel https://www.youtube.com/user/creativemindstz?feature=watch PART 1 (WATCH HERE)

PART 2

BBA: HUDDAH na DENZEL OUT!

Washiriki wa shindano la Big Brother Africa The Chase Huddah wa Kenya na Denzel wa Uganda wamekuwa ni washiriki wa kwanza kuondolewa kwenye shindano hilo. Click here for more

SHOW YA JAY DEE SASA NI TAREHE 14.

Hii ni kwa mujibu wa Lady Jay Dee mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Twitter.