Hii ndiyo picha ya kwanza kabisa ambayo mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama alipost jana baada ya kujiunga na mtandao wa Instagram kwa mara ya kwanza jana.
Jun 28, 2013
Jun 20, 2013
NEYMAR NI JUSTINE BIEBER WA SOKA - JOE BARTON
Mchezaji mwenye vituko, mwingereza Joe Barton anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa akitokea QPR ya England, alimnanga mchezaji chipukizi wa Brazil Neymar kupitia ukurasa wake wa Twitter mwezi March mwaka huu mara tu baada ya mechi kati ya Brazil na Urusi kwenye uwanja wa Stamford Bridge jijini London.
Kwenye mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya 1-1, Neymar hakucheza vizuri na Barton akatumia nafasi hiyo kumpondea bwana mdogo kwa kumuita Justine Bieber wa soccer, kwamba anaonekana anajua sana kwenye You tube lakini katika hali halisi hana kitu (mavi ya paka).
Miezi takribani mitatu baadye, jana usiku kwenye mechi ya robo fainali ya kombe la mabara, Neymar alicheza vizuri sana na kuiongoza Brazil kushinda 2-0 dhidi ya Mexico huku yeye akifunga bao la kwanza na kutengeneza la pili. Baada ya mechi hiyo, mchezaji mwenzake wa Brazil, Oscar Dos Santos anayechezea klabu ya Chelsea aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kama kumjibu Joe Barton.
Jun 19, 2013
VIDEO: MNYIKA AKIELEZA KUWA MLIPUAJI BOMU KWENYE MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA NI POLISI.
Video ikimuonesha Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA Mhe. John Mnyika akizungumza na Waandishi wa Habari tarehe 18/06/2013 Makao Makuu ya CHADEMA. Mnyika amesema CHADEMA inao ushahidi wa video kuwa aliyelipua bomu kwenye mkutano wa Chadema Arusha ni Polisi na Polisi wenzake wakamsaidia kutoroka.
Tazama video hii hapa chini
NAH-REEL AKIZUNGUMZIA KIFO CHA LANGA KUTOKA NCHINI UGANDA
Producer Nah-Reel akiwa nchini Uganda kwenye ziara ya
ku-promote ngoma ya HOLD ME BACK pamoja na kundi lake la NAVY-KENZO, amezungumzia kifo cha mwana Hip-Hop Langa Kileo.
Tazama video hapo chini.
SNURA KUZINDUA "MAJANGA" LEO HOTMIX EATV!
Snura (kulia) na Wema (kushoto) |
Mkali wa filamu za Bongo Snura ambaye hivi karibun ameingia kwenye fani ya muziki na kufyatua ngoma yake maarufu kama "Majanga", leo anatarajiwa kuzindua video ya wimbo huo kupitia kipindi cha HOTMIX kinachorushwa na EATV.
Swali kubwa, Je, video hiyo pia ni majanga? Yetu macho!
Jun 11, 2013
RAPA 2-CHAINZ AVAMIWA NA KUPORWA MCHANA KWEUPE, ATIMKA MBIO "KAMA MENDE AKIMBIAVYO MWANGA WA TAA"
Ripoti kutoka San Francisco Police Department zinasema kwamba rapper 2-Chainz aliporwa 'kweupe' majira ya saa kumi jioni, Jumapili ya Juni 9.
Polisi wanadai kuwa video za 'surveillance' zinaonesha kuwa rapa huyo na wenzake wapatao 14 walikimbia 'kama mende wakimbiavyo mwanga wa taa' wakati wa tukio hilo ambapo rapa huyo na msafara wake walivamiwa na kumiminiwa risasi, na vibaka hao kuondoka na wallet, na cheni kadhaa za dhahabu. Hakuna aliyejeruhiwa.
Hata hivyo polisi wameeleza kwamba 2-Chainz alijieleza kwa polisi kuwa 'haikuwa ishu kubwa' kwake na angeweza kuimaliza, na alidai kuwa majambazi hayo walifanikiwa tu kumpora wallet.
Baadae jioni hiyo, rapa huyo ali-perform kwenye concert huko Bay, San Fransisco.
Jun 8, 2013
Jun 6, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)