Hii ndiyo picha ya kwanza kabisa ambayo mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama alipost jana baada ya kujiunga na mtandao wa Instagram kwa mara ya kwanza jana.
FULL MICHAPO
Jun 28, 2013
Jun 20, 2013
NEYMAR NI JUSTINE BIEBER WA SOKA - JOE BARTON
Mchezaji mwenye vituko, mwingereza Joe Barton anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa akitokea QPR ya England, alimnanga mchezaji chipukizi wa Brazil Neymar kupitia ukurasa wake wa Twitter mwezi March mwaka huu mara tu baada ya mechi kati ya Brazil na Urusi kwenye uwanja wa Stamford Bridge jijini London.
Kwenye mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya 1-1, Neymar hakucheza vizuri na Barton akatumia nafasi hiyo kumpondea bwana mdogo kwa kumuita Justine Bieber wa soccer, kwamba anaonekana anajua sana kwenye You tube lakini katika hali halisi hana kitu (mavi ya paka).
Miezi takribani mitatu baadye, jana usiku kwenye mechi ya robo fainali ya kombe la mabara, Neymar alicheza vizuri sana na kuiongoza Brazil kushinda 2-0 dhidi ya Mexico huku yeye akifunga bao la kwanza na kutengeneza la pili. Baada ya mechi hiyo, mchezaji mwenzake wa Brazil, Oscar Dos Santos anayechezea klabu ya Chelsea aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kama kumjibu Joe Barton.
Jun 19, 2013
VIDEO: MNYIKA AKIELEZA KUWA MLIPUAJI BOMU KWENYE MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA NI POLISI.
Video ikimuonesha Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA Mhe. John Mnyika akizungumza na Waandishi wa Habari tarehe 18/06/2013 Makao Makuu ya CHADEMA. Mnyika amesema CHADEMA inao ushahidi wa video kuwa aliyelipua bomu kwenye mkutano wa Chadema Arusha ni Polisi na Polisi wenzake wakamsaidia kutoroka.
Tazama video hii hapa chini
Subscribe to:
Posts (Atom)