HOME

Apr 17, 2013

LULU MICHAEL BIRTHDAY BASH!!

Enzi hizoo na alivyo sasa
With her little bro
.......With Dk. Cheni
......Hot Lulu Michael
......With Ally Kiba
...With Her Friend
...With Another Beautiful friend

....Mama ake' ''Mama Lulu''
Kupitia page yake ya Instagram, Elizabeth Michael @Hotlulumichael ambaye ni Diva wa Tanzania Film Industry, ameamua ku share picha kadhaa za mambo tofauti yaliyojiri katika siku yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza umri wa miaka 18, Party iliyofanyika pale Serena Hotel Dar es salaam nchini Tanzania.

Lulu alionekana kuwa mwenye furaha iliyopitiliza haswa ukizingatia alikuwa huru uraiani lakini pia alikuwa akitimiza rasmi umri wa miaka 18 ambao anaingia utu uzima na kuwa kuwa na rights zote za kupiga kura.

Lulu aliwashukuru marafiki zake wote mostly walio show up katika party hiyo @ Thank u ma pipo....!!!i wnt stop saying dic word....!!!thank you soooo much.... Picha kamili  kama zinavyojieleza . Enjoy!!

POLISI UGANDA KUPAMBANA NA UGAIDI!!

Mkurugenzi wa rasilimali watu katika jeshi la polisi nchini Uganda Charles Birungi amesema kuwa jeshi la nchi hiyo lipo tayari katika kukabiliana na shambulizi lolote la kigaidi kama lililotokea Julai 2010.

Bw. Birungi amesema kuwa pia jeshi la polisi linaendelea na mchakato wa kujiweka tayari kupambana na shambulio lolote la kigaidi.

Ameweka wazi kuwa mashambulizi yoyote ya baadae katika nchi hiyo yatakabiliwa kwa kutumia teknologia na wanajeshi waliopatiwa mafunzo vizuri.

16 WAFA KWA KUANGUKIWA NA MGODI!!

Shirika la habari la BBC limeripoti kuwa, Takriban watu 16 wamefariki baada ya kuangukiwa na mgodi ambao ulikuwa hautumiki nchini Ghana.

Maafisa wamesema kuwa kulikua na maporomoko ya ardhi katika sehemu ambayo ilikua haitumiki karibu na mji wa Kyekyewere ambao una sifa ya kuwa na wachimbaji haramu wa migodi.

Kwa mujibu wa maafisa wakuu, Waokoaji waliondoa miili 16 baada ya mgodi huo kuporomoka siku ya Jumatatu.

Haijulikani idadi ya watu waliokuwemo ndani ya mgodi huo , lakini imedaiwa kuwa hakuna dalili kuonyesha kuwa bado kuna miili mingine ndani ya mgodi huo.

Afisa mmoja ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa mchimbaji mmoja aliyekuwa amejeruhiwa alifariki baadaye hospitalini. Hii inaongeza idadi ya waliofariki hadi 17.

Apr 16, 2013

DEADLY BOSTON BLASTS!!




Google inachukua hatua kuwasaidia wanariadha kuwapata wapendwa wao waliopotea kutokana na mashambulizi huko Boston karibu na mstari wa kumalizia mbio ndefu.

Mtandao huo unaoitwa Google Person Finder,unamruhusu mtumiaji kuingiza jina la mtu anayemtafuta au kuingiza taarifa kuhusu mtu ambaye yupo katika eneo la tukio.

Mawasiliano ya simu yamekuwa magumu katika eneo la Boston ambapo makampuni ya simu yamesema imekuwa vigumu huduma kupatikana lakini ni kutokana na foleni kubwa iliyopo.