HOME

Jun 3, 2013

TAIFA STARS 0 - 0 SUDAN (02.06.2013)


Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars jana mjini Addis Ababa Ethiopia ilitoka suluhu na Sudan katika mechi ya kujipima nguvu kuelekea kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil 2014.

Katika mchezo huo, Stars iliwakosa nyota wake Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao jana nao walikuwa na kibarua wakiitumikia timu yao ya TP Mazembe huko mjini Maputo katika michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Liga Muculumana ya Msumbiji.

Stars inatarajiwa kukipiga na Morocco huko mjini Marakesh, Morocco Jumamosi tarehe 8.

No comments:

Post a Comment