HOME

Jun 11, 2013

RAPA 2-CHAINZ AVAMIWA NA KUPORWA MCHANA KWEUPE, ATIMKA MBIO "KAMA MENDE AKIMBIAVYO MWANGA WA TAA"


Ripoti kutoka San Francisco Police Department zinasema kwamba rapper 2-Chainz aliporwa 'kweupe' majira ya saa kumi jioni, Jumapili ya Juni 9.

Polisi wanadai kuwa video za 'surveillance' zinaonesha kuwa rapa huyo na wenzake wapatao 14 walikimbia 'kama mende wakimbiavyo mwanga wa taa' wakati wa tukio hilo ambapo rapa huyo na msafara wake walivamiwa na kumiminiwa risasi, na vibaka hao kuondoka na wallet, na cheni kadhaa za dhahabu. Hakuna aliyejeruhiwa.

Hata hivyo polisi wameeleza kwamba 2-Chainz alijieleza kwa polisi kuwa 'haikuwa ishu kubwa' kwake na angeweza kuimaliza, na alidai kuwa majambazi hayo walifanikiwa tu kumpora wallet.

Baadae jioni hiyo, rapa huyo ali-perform kwenye concert huko Bay, San Fransisco.

No comments:

Post a Comment