HOME

Jun 20, 2013

NEYMAR NI JUSTINE BIEBER WA SOKA - JOE BARTON

Mchezaji mwenye vituko, mwingereza Joe Barton anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa akitokea QPR ya England, alimnanga mchezaji chipukizi wa Brazil Neymar kupitia ukurasa wake wa Twitter mwezi March mwaka huu mara tu baada ya mechi kati ya Brazil na Urusi kwenye uwanja wa Stamford Bridge jijini London. 

Kwenye mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya 1-1, Neymar hakucheza vizuri na Barton akatumia nafasi hiyo kumpondea bwana mdogo kwa kumuita Justine Bieber wa soccer, kwamba anaonekana anajua sana kwenye You tube lakini katika hali halisi hana kitu (mavi ya paka).



Miezi takribani mitatu baadye, jana usiku kwenye mechi ya robo fainali ya kombe la mabara, Neymar alicheza vizuri sana na kuiongoza Brazil kushinda 2-0 dhidi ya Mexico huku yeye akifunga bao la kwanza na kutengeneza la pili. Baada ya mechi hiyo, mchezaji mwenzake wa Brazil, Oscar Dos Santos anayechezea klabu ya Chelsea aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kama kumjibu  Joe Barton.


No comments:

Post a Comment