![]() |
Hamilton alijirusha kinyume nyume kwenye bwawa la kuogelea ikiwa ni staili ya kusherekea ushindi |


Dereva wa McLaren Lewis Hamilton jana aliibuka mshindi wa mpambano wa Canadian Grand Prix na michuano hiyo ya mwaka huu imekuwa ikimpata mshindi tofauti tangu ilipoanza msimu huu.
Hamilton alipambana kutoka nafasi ya tatu na kuwapita Fernando Alonso na Sebastian Vettel katika mizunguko ya mwisho ya mpambano huo.
Mkakati wa Alonso kusimama mara moja haukumsaidia na kujikuta akiporomoka kutoka kileleni na kumaliza akiwa wa tano baada magurudumu ya gari lake kuonyesha dalili za kutostahimili.
No comments:
Post a Comment