HOME

Jan 6, 2012

FEDERER,NADAL WATINGA NUSU FAINALI QATAR!

Roger Federer

Rafael Nadal
Bingwa mtetezi wa shindano la wazi la Qatar Roger Federer amemfunga kwa seti  6-3, 5-7, 6-4  Andreas Seppi wa Italia na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.


Naye mchezaji namba moja kwa ubora duniani Rafael Nadal  ametinga nusu fainali baada ya kumfunga Mikhail Youzhny wa Urussi kwa seti 6-4, 6-4 ,Nadal atakumbana na mfaransa Gael Monfils katika nusu fainali hiyo,Monfils alimfunga Victor Troicki kwa seti 6-2, 6-3. .


Federer atakumbana na mfaransa mwingine Jo-Wilfried Tsonga, ambaye alimfunga katika fainali za tour ya dunia ATP,lakini alifungwa na Tsonga katika robo fainali ya shindano la Wimbledon.

No comments:

Post a Comment