![]() |
Manny Pacquiao (kulia) |
Bingwa wa ngumi Manny Pacquiao amepewa uchaguzi wa kuchagua bondia kati ya wanne atakayepigana naye katika pambano lijalo lakini siyo bondia nguli Floyd Mayweather ambaye anatarajia kuanza kutumikia kifungo jela leokwa siku 90.
Mabondia ambao wametajwa ni Juan Manuel Marquez wa Mexico, Miguel Cotto wa Puerto Rico na mabondia wa Marekani Timothy Bradley na Lamont Peterson.
Mdhamini wa masumbwi Bob Arum amesema ataweka kila kitu kwa ajili ya Manny Pacquiao kuchagua.
No comments:
Post a Comment