Rais wa CWT Bw. Gratian Mukoba (kulia)
Chama cha walimu Tanzania (CWT) kimetangaza kusitisha mgomo uliokuwa uanze Januari 9 mwaka huu siku ya Jumatatu kuishinikiza serikali kulipa madeni yao yanayofikia shilingi bilioni hamsini na tatu.
Rais wa chama hicho Bw. Gratian Mukoba amesema hatua ya kusitisha mgomo huo inatokana na serikali kuanza kulipa madai yasiyohusu mishahara yanayofikia shilingi bilioni 22.25.
Kwa mujibu wa Bw. Mukoba, mbali na kuanza kulipa madeni hayo, serikali pia imefuta waraka alioudai kuwa ni kandamizi na uliokuwa unarudisha nyuma maslahi ya walimu nchini.
No comments:
Post a Comment