HOME

Jan 5, 2012

WIZARA YA AFYA KUKUSANYA VIPIMO VYA UKIMWI VILIVYOPIGWA MARUFUKU

 vipimo vya SD Bioline

Wizara ya afya na ustawi wa jamii imeanza kukusanya na kuvirejesha katika bohari kuu ya dawa (MSD) iliyopo jijini Dar es Salaam vipimo vyote aina ya SD Bioline vinavyotumika kupimia virusi vya ukimwi, ambavyo shirika la afya ulimwenguni WHO imepiga marufuku matumizi yake siku za hivi karibuni.

Msemaji wa wizara ya afya Bw. Nsachris Mwamwaja, amesema MSD itaviteketeza vipimo hivyo mara baada ya zoezi la kuvikusanya kutoka katika hospitali na vituo mbali mbali vya afya kukamilika.

Hatua ya wizara ya afya imekuja baada ya shirika la afya duniani (WHO) kuzuia ununuzi, usambazaji na utumiaji wa vipimo hivyo vinavyotumika kutoa majibu ya haraka ya vipimo vya ukimwi, baada ya uchunguzi kubaini kuwa vinatoa majibu yasiyo sahihi.

No comments:

Post a Comment