HOME

Jan 8, 2012

SERIKALI IMEKANUSHA KUWAFUKUZA MADAKTARI WA MAFUNZO KWA VITENDO MUHIMBILI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni.


Serikali ya Tanzania imesema haijawafukuza madaktari walio katika mafunzo ya vitendo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) waliogoma hivi karibuni na wala haina mpango wa kama huo.


Hayo yamesema na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni.


Katibu huyo amelazimika kutoa ufafanuzi huo kutokana na vyombo kadhaa vya habari
kuripoti kuwa, madaktari 229 walio katika mafunzo ya vitendo katika hospitali ya Muhimbili wamefukuzwa kutokana na kufanya mgomo wa nchi nzima kwa lengo la kushinikiza serikali kuwalipa malimbikizo ya posho zao yanayofikia Sh milioni 176.

No comments:

Post a Comment