HOME

Jan 8, 2012

NIGERIA YAENDELEA KUKUMBWA NA MASHAMBULIZI



Picha za magari yaliyochomwa moto

Miili ya watu waliouwawa katika mashambulizi hayo


Nigeria imeendelea kukumbwa na wimbi la machafuko ambayo yamelenga jamii ya wakristo nchini humo,ambapo waru 17wameuwawa huko katika Mubi jimbo la Adamawa baada ya mtu mmoja mwenye silaha kuwashambulia wakristo katika jengo moja walikokuwa wakikutana.


Kumekuwa na taarifa nyingine ya mashambulizi mabaya katika mji mkuu wa Adamawa wa Yola ambapo kundi la waislamu la Boko Haram limesema kuwa lilifahya mashambulizi huko Mubi na Gombe siku ya Alhamisi usiku ambapo watu sita waliuwawa.


Kundi hilo limeendelea kufanya mashambulizi huko kaskazini na kati nchini Nigeria katika miezi ya hivi karibuni ikiwa ni pamoja siku ya kristmasi ambapo kundi hilo lilifanya shambulio katika kanisa karibu na mji mkuu wa Abuja na kuuwa watu wengi.

No comments:

Post a Comment