![]() |
Azam Fc |
Leo ni leo Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar wakati Simba na Azam zitakaposhuka dimbani katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Simba imeingia hatua hiyo baada ya kushika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Jamhuri, wakati Azam imeongoza kwenye kundi mbele ya Mafunzo.
Ni mchezo unaokutanisha timu mbili zinazofahamiana vizuri, ambapo zote zinashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na mara nyingi zinapokutana mchezo huwa wa ushindani mkubwa.
No comments:
Post a Comment