HOME

Jan 9, 2012

AJALI YAUA WATU SABA NCHINI UGANDA!!

Basi la Gaagaa

Watu saba wamefariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia ajali ya basi lenye jina la Gaagaa lililokuwa likitoka Lira kwenda jijini Kampala nchini Uganda kuligonga gali la mizigo lililokuwa limesisimama katika eneo la Kalule barabara kuu ya Bombo-Gulu.


Kwa mujibu wa gazeti moja la nchini humo watu watano wamekufa papo hapo wakati wengine wawili walikufa baada ya kufikishwa katika hospitali ya rufaa ya taifa ya Mulago jijini Kampala katika ajali hiyo iliyotokea mapema leo alfajiri.


Taarifa hiyo imesema kati ya watu waliokufa ni pamoja na askari magereza Susan Akello na Betty Dora na askari polisi ambaye ametambulika kwa jina la Emmanuel Lwanga ambaye alikuwa akilinda gari hilo la mizigo lililokuwa limesimama.

No comments:

Post a Comment