Baraza la habari nchini Tanzania (MCT) limekea vikali baadhi ya vyombo vya habari kutokana na ilichodai kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya uandishi wa habari wakati vikiripoti kukamatwa na hatimaye kufikishwa mahakamani kwa msanii wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama LULU.
Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya MCT, jaji mstaafu Thomas Mihayo amesema idadi kubwa ya vyombo vya habari, hususani magazeti vimeandika habari hiyo vikimtia hatiani LULU kuwa amehusika na kifo cha msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba hata kabla mahakama haijathibitisha tuhuma hizo.
Aidha kwa upande wake, katibu mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga amesema kitendo kilichofanywa na vyombo hivyo vya habari ni hatari kwa maisha ya mtuhumiwa kwani jamii hivi sasa inamuangalia msanii huyo kwa jicho baya kutokana na kuamini sana taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment