Mar 10, 2012
SERIKALI YAPANIA KUWADHIBITI WANAOOA WANAFUNZI!!
Wanawake Mkoani Arusha nchini Tanzania wametakiwa kutokubali kurubuniwa kwa kuwaficha wanaume wanaowaoa mabinti zao walioko shule za msingi na sekondari na badala yake kuwafichua ili kuwezesha serikali kukomesha tabia hiyo
Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kwa mkoa wa arusha yalifanyika katika mji mdogo wa mto wa mbu uliopo katika wilaya ya Monduli
Mulongo ameeleza kuwa wanawake wengi vijijini wamekuwa wakirubuniwa kwamba kwa kuwafichua wanaume wanaooa ama kuwapa mimba mabinti zao kuwafanya wakose wakwe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment