Mayor wa manispaa ya Ilala .Jerry Silaa |
Senior Sales Manager wa Serena Hotel,Ailena Mhanga. |
Muandaaji Wa Fashion For Floods Mustafa Hassanali |
Mbunifu mahiri wa mavazi Tanzania Mustapha Hassanali, pamoja na Meya wa manispaa ya Ilala, Mheshimiwa Jerry Slaa, wamejiunga pamoja ili kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea Desemba Jijini Dar es Salaam, kupitia onyesho la mavazi litakalofanyika tarehe 12 mwezi huu.
Mustafa amesema kuwa sababu kubwa ya kuandaa tukio hili ni kutokana na kuguswa na janga hili la mafuriko lililowaathiri wakazi wa Dar es Salaam, hususan wale wanaoishi mabondeni ambao ni watanzania wenzetu.
Pia, Mustafa ametoa wito kwa wale wote ambao pia wameguswa na hali inayowakabili waathirika wa mafuriko, kuhudhuria maonyesho haya na kuwa moja ya washiriki katika kuwafariji waathirika hawa na kufanya kazi pamoja katika kuleta madiliko katika maisha ya wale walioathirika na janga hilo.
No comments:
Post a Comment