HOME

Jan 10, 2012

FILAMU YA MAISHA YA MANDELA YAANDALIWA

Nelson Mandela na mkewe

Mfululizo wa vipindi vifupi vya televisheni kuhusu maisha ya Nelson Mandela viko njiani kutayarishwa huku kati ya waandaaji yuko mjukuu wa Rais huyo wa zamani.


Waandishi walio katika mradi huo ni pamoja na Nigel Williams, aliyeandika vipindi vya Helen Mirren mwaka 2005, Elizabeth I.


Mandela na familia yake atatoa taarifa na mrisho nyuma wa muswada katika sehemu ya sita ya mfululizo huo.


Mjukuu wake Kweku Mandela amesema mwitikio wa babu yake alipoelezwa kuhusu mpango huo ulikuwa: "Nitalipwa kiasi gani?"


Upigaji picha utaanza Afrika Kusini baadaye mwaka huu.


Vitabu viwili vya Nelson Mandela vitatumika kama vyanzo vikuu vya taarifa – chenye rekodi binafsi cha ‘Conversations With Myself’ na kile chenye nukuu ya matamshi yake ‘Nelson Mandela By Himself.’

No comments:

Post a Comment